Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kipigo hicho kimeididimiza Man United chini zaidi na kudhihirisha wazi kwamba, kocha wao wa sasa Ole Gunnar Solskjaer si mtu sahihi wa kuendelea kufanya kazi kwenye kikosi hicho ambacho hali yao imezidi kuwa mbaya siku hadi siku.
 
Ndani ya muda huo, Man United imezidiwa pointi hadi na Wolves, Crystal Palace na Everton, huku yenyewe ikijivunia tu kuzipiku pointi timu za Newcastle, Burnley, Arsenal na Southampton tena si nyingi, pointi mbili tu jambo linalozifanya timu hizo kujiona kuwa zipo kwneye daraja moja na miamba hiyo ya Old Trafford baada ya kuwa chini ya Solskjaer.
 
Makali ya Liverpool si mchezo kwenye Ligi Kuu England. Kwa kuanzia Machi 28, 2019 wababe hao wa Anfield wanaonolewa na Jurgen Klopp wamevuna pointi nyingi kuliko timu nyingine yoyote, ambapo kwenye mechi 29 walizocheza wamevuna pointi 85, wakishinda 28, sare moja na hawajapoteza mchezo wowote.
 
Man City - mechi 32, pointi 75

Tangu Solskjaer alipokabidhiwa mikoba ya kudumu huko Man United, mahasimu wao Manchester City wameshuka uwanjani mara 32 kwenye mechi za Ligi Kuu England na kuvuna pointi 75. Katika mechi hizo, Man City imeshinda 24, sare tatu na kupokea vichapo vitano, huku ikifunga mabao 81 na kuruhusu nyavu zao kuguswa mara 29. Kwa kuanzia muda huo Man City ni ya pili kwa pointi. Msimu uliopita, Man City ilibeba taji lake la pili mfululizo kwenye ligi, lakini msimu huu ngoma imekuwa ngumu mbele ya Liverpool wasioshindika.
 
Leicester City - mechi 31, pointi 59

Liverpool na Manchester City zimeweka pengo kubwa sana la pointi kwa hesabu za kuanzia alipopewa ajira ya kudumu kocha Solskjaer huko Old Trafford. Timu inayoshika nafasi ya tatu kwa kuvuna pointi nyingi ndani ya muda huo ni Leicester City, iliyocheza mechi 31 na kuvuna pointi 59. Katika mechi hizo, Leicester imeshinda mechi 18, sare tano na kuchapwa nane, huku ikiwa imefunga mabao 63 na kufungwa 29. Sasa chama hilo la Brendan Rodgers linawania kumaliza ndani ya Top Four.
 
Chelsea - mechi 32, pointi 55

Baada ya kuondoka Maurizio Sarri aliyemalizia msimu uliopita huko Stamford Bridge, Frank Lampard ametua kuchukua mikoba ya kuinoa Chelsea. Kwa kuanzia Machi, ambapo Solskjaer alikabidhiwa mikoba ya kudumu ya kuinoa Man United, Chelsea yenyewe imecheza mechi 32 na kuvuna pointi 55. Ndani ya muda huo, The Blues imeshinda mechi 16, sare saba na vichapo tisa, huku ikiwa na mabao 54 ya kufunga na 38 ya kufungwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…