Wako kama panzi. Nguvu yao kubwa ipo kwenye namba. Yaani kundi moja (swarm) wanaweza kuwa hata milioni kadhaa yaani wakisafiri wanaweza hata kuziba mwanga wa jua kukawa na giza. Pale watakaposhukia basi kazi yao ni kula tu usiku na mchana na kumaliza kila kitu.
Kuwadhibiti ni kuharibu sehemu yao ya kuzaliana na kuwaua kwa madawa (fumigation) na kuwaangamiza kimoja japo wataalamu wanasema kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea duniani mambo kama haya yatakuwa ya kawaida tu.
Ukiongea na wazee mabaa mengi ya njaa hapo zamani yalisababishwa na nzige. Ni wadudu wa hatari na sijui Wakenya wamejipangaje. Hata sisi sijui tumejipangaje kwa sababu watakuja tu....