Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KUNA jina jipya katika tenisi ya wanawake duniani, wakati kizazi cha kina Venus na Serena Williams kikielekea ukingoni, Coco Gauff anaibuka na kuja kwa kasi ambayo inawafanya wachambuzi wa mchezo huo kukubali kuwa ni tishio jipya.
 
Akiwa na umri wa miaka 15 tu, tayari Coco ni hatari na kila kukicha anaandika historia mpya huku akiwashangaza mastaa wenye majina makubwa kwa kuwapa dozi ambazo zinawafanya wabaki wakiwa hawaamini kama wameadhibiwa na mtoto mdogo.
 
Kiwango kizuri cha Coco katika michuano mbalimbali ya tenisi kimekuwa tiketi yake ya kupiga pesa ndefu kulinganisha na umri wake, kwani tayari licha ya kuwa na umri wa miaka 15 anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 2.5 milioni.
 
Coco anavyopiga Pesa
Coco alijitambulisha katika ulimwengu wa tenisi mwaka 2019 baada ya kumchapa Venus Williams kwenye michuano ya Wimbledon hadi akaingia katika michuano hiyo alikuwa na utajiri wa Dola 75,000, ushindi huo ukamhakikishia kupiga Dola 223,464.
 
Kwa upande wa mikataba ya udhamini, Coco ana mkataba na kampuni ya vifaa vya michezo ya New Balance, kampuni ya tambi ya Barilla na pia anadhaminiwa na kampuni ya kutengeneza vifaa vya kuchezea tenisi ya Head. Kwa ujumla anaingiza Dola 1 milioni kutokana na mikataba yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…