Kutokana na kufika hatua ya 16 bora ya michuano ya wazi ya tenisi ya Australia ya 2020 akiwatoa Venus na Naomi Osaka katika hatua za mwanzo za michuano hiyo, Coco amepiga Dola 300,000.
Mwaka jana aliingiza kiasi cha Dola 163,000 kutokana na kuishia katika hatua ya 32 bora ya michuano ya US Open. Kwa ujumla mwaka 2019 aliingiza jumla ya Dola 486,390.
Amezaliwa katika familia ya michezo, baba Corey Gauff aliwahi kucheza kikapu katika Chuo Kikuu cha Georgia wakati mama Candi Gauff alikuwa mwanariadha akishiriki mashindano kadhaa wakati akisoma Chuo Kikuu cha Florida.
Akiwa na miaka 11, kocha wa Serena Williams alimpa nafasi ya kushiriki kambi ya tenisi iliyofanyika Nice, Ufaransa huku akicheza mechi ya kwanza kama mchezaji wa kulipwa Mei 2018 katika mashindano yaliyofanyika Osprey, Florida.