Kuangalia kipindi cha TV unachokipenda zaidi, au kwenda kutembea sehemu unayoipenda. Kama unaweza kila siku fanya kitu au kitendo ambacho kitawafurahisha wengine. Mfano inaweza kuwa ni neno, kuwasaidia wanafunzi wenzako au wafanyakazi wenzako, kusimamisha gari yako kuruhusu watu wavuke, kumpisha mtu katika kiti ndani ya gari, au kumpa zawadi hata kama ndogo tu Yule unayempenda. Unapomfanya mtu kuwa na furaha, wewe pia vilevile utakuwa na furaha, na watu watajitahidi kukufanya uwe na furaha.