Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama mvi ni kipimo cha busara.......... Kwa nini zifichwe?

Kwa zamani ingekuwa ni muhali mkubwa mtu kuuliza swali la aina hii, kwa sababu mvi zinahesabiwa kama dalili ya busara, bila shaka zikihusianishwa na kuona mengi ambayo ni wenye umri mkubwa tu waliokuwa na nafasi hiyo. Lakini leo, mvi ni kisirani na karibu kila mtu anajaribu kuzikimbia, kwani kuendalea kuwa kijana ni sifa kubwa. Kwa sasa uzee unanuka na kila mmoja anajaribu kuukimbia kwa njia mbalimbali ikiwemo ya kukana umri na kujirudisha nyuma kimatendo. Kwa kifupi hii ndiyo historia ya mvi, usiziogope bure!
 
Karibu rangi zote asilia za nywele zinatoka kwenye kitu kiitwacho melanin, ambacho huzalishwa na mwili kutokana na seli zinazofahamika kama melenocytes. Nywele zinapobadilika na kuwa nyeupe ina maana kwamba, melenocytes haizalishi tena melanin. Mabadiliko haya ya nywele kutoka rangi nyeusi na kukosa rangi (mvi) siyo hatua ya siku moja bali mwaka na miaka, kwani nywele moja hubadilika baada ya muda mrefu na nyingine na nyingine. Siyo hatua ya siku moja tu. Kwa kadiri mtu anavyozeeka ndivyo ambavyo uwezo wa mwili kuzalisha melanin unavyopungua.
 
Uwezo huu huanza kupungua mtu anapofikia umri wa miaka 35 au 40. Lakini watu wengine huanza kuota mvi wakiwa na umri wa miaka hata 20 tu. Je, hii nayo inatokana na nini?Pengine ni jambo la ajabu kwamba kuvuta sigara kunatajwa kama sababu ya kuchochea mtu kupata mvi akiwa na umri mdogo. Ukiwachunguza wavuta sigara wazuri, utagundua kwamba wameanza kuota mvi mapema kuliko umri wa miaka 35 au 40. Matatizo kwenye kiungo kinachodhibiti ukuaji mwilini, yaani thyroid huweza pia kusababisha mtu kupata mvi kabla ya kufikisha umri wa miaka 35. Pia ukosefu wa vitamin B12 unatajwa kwa sababu nyingine.Kuna watu ambao hata kama wana umri wa miaka 60 bado hawataki kuona nywele nyeupe vichwani mwao .
 
Watu hawa huangaika huku na kule kutafuta dawa kuondoa mvi na pengine kutumia rangi ya nywele ili kufanya rangi ya nywele nyeupe zisionekane. Huu ni kama mwendawazimu kwa kiasi fulani. Kwanini? Kwanza kuna ukweli kwamba nyingi kati ya hizo zinazodaiwa kuwa rangi za kuondoa mvi, zina athari katika mwili wa mtumiaji. Lakini wendewazimu mkubwa zaidi ni kitendo chao cha kukataa ukweli ambao inabidi wajivunie.Mvi bado ni dalili ya busara. Kama umefikia umri wa kuota mvi na hujafanya jambo lolote la maana na hujatoa mchango wowote wa maana kwa familia yako au jamii unamoishi ni lazima utaficha mvi zako. Kwanini? Kwa sababu utaona haya sana kuonekana kwamba umri wako ni mkubwa lakini hujafanya lolote.
 
Ninaposema mchango wa maana sina maana ya fedha au mali, bali zaidi nina maana ya mawazo ya kujenga na pengine kuandaa misingi ya kujenga kwa nia ya kuleta maendeleo baadaye. Hebu chunguza kwa makini, utagundua kwamba watu wote wanaojaribu kuficha mvi ni wale watu ambao wametawaliwa sana na vionjo na tamaa ya miili yao kuliko maendeleo ya binadamu. Ni wale watu ambao hata kama wana fedha, hawajajua hasa wako hapa duniani kwa sababu gani. Hivi ndivyo ilivyo kwa sababu watu wa aina hii huhofia sana umri, huhofia sana kufa kwa sababu hawajakamilisha walichokuja kukifanya duniani kwasababu hawajajua bado.
 
Kinywaji cha viungo:
Hiki ni kinywaji chochote ambacho kimetengenezwa kwa kuwekwa viungo. Kinywaji hiki kinaweza kuwa cha moto au cha baridi. Kinywaji cha baridi kinapotengenezwa, yatumike maji yaliyochemshwa.
 
Chai:
Hiki ni kinywaji ambacho hutengenezwa kwa kutumia maji ya moto na majani ya chai. Wakati mwingine sukari na maziwa huongezwa. Mara nyingine watu wanapotengeneza vinywaji vya viungo huviita "chai" hata kama havina majani ya chai. Ukweli ni kwamba chai ni yale majani ya chai. Katika kijitabu hiki vinywaji vya viungo havikuitwa chai.
 
BAADHI YA VIUNGO, MATUMIZI NA FAIDA ZAKE

Kitunguu saumu (Garlic)
Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizi mbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo mara nyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache. Vingine ni vile vyenye
rangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogo na nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa.
 
Kitunguu saumu hufaa katika matatizo mengi kama kusaidia kuzuia maambukizi yatokanayo katika utumbo, mapafu na sehemu za ukeni. Vilevile husaidia katika uyeyushwaji wa chakula, kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani, maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi.
 
Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai au kinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguu saumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sita kwa siku hasa kama vitatumika vibichi .
 
Tangawizi (Ginger)
Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa tangawizi. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga. Ta n g a w i z i inaweza kutumika katika vinywaji vilivyochemshwa. Pia huweza kuongezwa kwenye vinywaji vingine au kwenye chakula.
 
Tangawizi husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza kichefuchefu, kutapika, kuharisha, maumivu ya tumbo na gesi tumboni. Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu.
 
Iliki (Cardamom)
Iliki ni mbegu zinazotokana na mmea wa iliki ambazo hutumika kama kiungo. Mbegu hizi huweza kusagwa au kutwangwa na kuongezwa kwenye chakula au katika vinywaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…