Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kombe la FA mara moja 2003–04, Kombe la Ligi mara mbili 2005–06, 2008–09, Ngao ya Jamii mara moja mwaka 2007, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara moja 2007–08, Kombe la Dunia la Klabu mara moja mwaka 2008.
 
Akiwa Real Madrid, amebeba La Liga mara mbili 2011–12, 2016–17, Kombe la Mfalme mara mbili, 2010–11 na 2013–14, Kombe la Super Cup ya Hispania mara mbili mwaka 2012 na 2017, Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne, 2013–14, 2015–16, 2016–17 na 2017–18, UEFA Super Cup mara mbili 2014 na 2017, Kombe la Dunia la Klabu 2014, 2016 na 2017.
 
Kwa upande wa Juventus ambako Juzi kati hapa ameweka rekodi ya kufunga mabao katika mechi 11 mfululizo ana taji moja la Serie A 2018–19 na Super Cup ya Italia moja mwak 2018.
 
Manchester United Euro 800.75 milioni

Manchester United ni moja kati ya klabu maarufu zaidi duniani, licha ya kutetereka katika miaka ya karibuni chini ya Kocha Ole Gunnar Solskjaer, bado ina wachezaji kibao wenye thamani kubwa.

Kikosi cha Man United kina thamani ya Euro 800.75 milioni na mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi pale Old Trafford ni Paul Pogba mwenye thamani ya Euro 100 milioni, akifuatiwa na Marcus Rashford, Euro 80 milioni.
 
Imewashangaza wengi msimu huu kutokana na kiwango chake. Licha ya kubadilisha kocha na kufungiwa kusajili, lakini The Blues wanapambana kumaliza miongoni mwa timu nne za juu katika Ligi Kuu England. Kikosi cha Chelsea kina thamani ya Euro 848.05 milioni na mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi ni N’Golo Kante ambaye thamani yake ni Euro 100 milioni, akifuatiwa na Jorginho Euro 65 milioni.
 
Atletico Madrid Euro 863.50 milioni

Atletico Madrid imeibuka na kumaliza utawala wa Real Madrid na Barcelona katika soka la Hispania. Diego Simeone ametengeneza kikosi cha wachezaji wenye viwango na amefanikiwa kushinda mataji kadhaa na timu hiyo. The Rojiblancos wana kikosi chenye thamani ya Euro 863.50 milioni na mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi kwenye kikosi chake ni Jan Oblak na Joao Felix ambao wote wana thamani ya Euro 100 milioni.
 
Tottenham Euro 897.50 milioni

Tottenham ina kikosi chenye thamani ya Euro 897.50 milioni, usajili mpya na kuondoka kwa baadhi ya wachezaji ndiyo kunaiweka Spurs katika nafasi hii. Kuondoka kwa Christian Eriksen kumeifanya timu hiyo kupunguza thamani ya Euro 85 milioni, lakini ujio wa Gedson Fernandes na Steven Bergwijn umeziba mapengo. Mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi katika kikosi cha Spurs ni Harry Kane ambaye thamani yake ni Euro 150 milioni, akifuatiwa na Dele Alli, Euro 90 milioni, Heung-min Son, Euro 80 milioni.
 
Bayern Munich Euro 934.15 milioni

Bayern Munich ndiyo timu pekee kutoka Ujerumani katika orodha hii, ikiwa na kikosi chenye thamani ya Euro 934.15 milioni. Serge Gnabry na Joshua Kimmich ndiyo wachezaji wenye thamani kubwa zaidi katika kikosi hiki akiwa na thamani ya Euro 80 milioni, kisha anafuatiwa Philippe Coutinho, Robert Lewandowski na Lucas Hernandez, Euro 70 milioni.
 
Paris Saint-Germain Euro 1.02 bilioni

Paris Saint-Germain ndiyo timu bora zaidi kwenye makaratasi. Ikiwa na safu ya ushambuliaji yenye mastaa kama kina Neymar Jr, Kylian Mbappe, Edinson Cavani, Angel di Maria na Mauro Icardi, unaweza kupata picha jamaa ni wakali kiasi gani.
 
Kikosi chao kina thamani ya Euro 1.02 bilioni, huku Mbappe ndiye mchezaji mwenye thamani zaidi, sokoni thamani yake ni Euro 200 milioni, akifuatiwa na Neymar Euro 160 milioni.
 
FC Barcelona Euro 1.07 bilioni

Katika kikosi cha Barcelona kuna mchezaji bora zaidi duniani kwa sasa, Lionel Messi na timu hiyo inathamani ya Euro 1.07 bilioni, huku uwepo wa mastaa kama kina Antoine Griezmann na Frenkie de Jong kukichangia kupandisha thamani ya klabu hiyo.
 
Messi ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi Barcelona akiwa na thamani ya Euro 140 milioni, wakati Griezmann ana Euro 120 milioni, huku De Jong na Marc-Andre Ter Stegen wote wakiwa na Euro 90 milioni.
 
Real Madrid Euro 1.08 bilioni

Real Madrid ni moja kati ya klabu bora zaidi ya karne ya 21. Thamani ya kikosi cha Zinedine Zidane ni Euro 1.08 bilioni. Eden Hazard ndiye mchezaji ghali zaid akiwa na thamani ya Euro 120 milioni.
 
Liverpool Euro 1.19 bilioni

Jurgen Klopp ndiye mtu ambaye ameifufua Liverpool yenye kikosi chenye thamani ya Euro 1.19 bilioni, huku mastaa ambao wana thamani kubwa kwenye kikosi hicho wakiwa ni pamoja na Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino, huku Mane na Salah wakiwa na thamani ya Euro 150 milioni kila mmoja na Firmino 90 milioni.
 
Manchester City Euro 1.29 bilioni

Manchester City ndiyo timu yenye kikosi chenye thamani kubwa zaidi duniani chini ya Kocha Pep Guardiola. Thamani ya timu hiyo ni Euro 1.29 bilioni. Na mchezaji ghali ni Raheem Sterling, Euro 160 milioni akifuatiwa na Kevin de Bruyne, Euro 150 milioni.
 
Manchester City Euro 1.29 bilioni

Manchester City ndiyo timu yenye kikosi chenye thamani kubwa zaidi duniani chini ya Kocha Pep Guardiola. Thamani ya timu hiyo ni Euro 1.29 bilioni. Na mchezaji ghali ni Raheem Sterling, Euro 160 milioni akifuatiwa na Kevin de Bruyne, Euro 150 milioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…