Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matumizi mazuri ya pesa

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kuwa kuweka akiba siyo kuwa na pesa nyingi bali ni maamuzi na mipango stahiki pekee.Hivyo kuweka akiba kutakufaidisha kwa kukuwezesha kutumia pesa vyema. Ikiwa unapata elfu kumi kwa siku, itakubidi uitumie vizuri ili uweze kutenga fedha ya akiba.Kama huweki akiba huna haja ya kutumia pesa vyema kwani hakuna sehemu ya akiba inayotakiwa kutengwa.
 
Kujiaandaa kwa dharura

Watu wengi huingia kwenye madeni au kupata uhitaji mkubwa wa pesa mara wapatwapo na dharura. Hivyo kwa kuweka akiba utapata faida ya kukuepushia mahangaiko wakati wa dharura kama vile maradhi, msiba, majanga, n.k.
 
Kuweza kufanya manunuzi au miradi ya gharama kubwa

Kuna manunuzi au miradi ambayo inahitaji pesa nyingi ili kuitekeleza. Maswala kama vile ujenzi wa nyumba, ununuzi wa kiwanja, kununua gari, n.k. ni baadhi ya mambo yanayohitaji fedha nyingi.Hivyo, kwa kuwa na akiba utaweza kutekeleza mambo haya kwa urahisi zaidi kuliko ungeyafanya bila akiba.
 
Kuweza kumudu wanaokutegemea

Ikiwa kuna watu wanaokutegemea kama vile wazazi, ndugu au watoto; ni vyema kuweka akiba ili uweze kuwa na fedha ya kukidhi mahitaji yao mara wapatwapo na uhitaji.Kutokuweka akiba kutakufanya uhangaike huku na huko ukitafuta fedha za kukidhi mahitaji ya wategemezi wako kama vile chakula, matibabu au hata ada za shule.
 
Utulivu wa akili

Unapokuwa huna akiba yoyote huwezi kuwa na utulivu wa akili. Kila wakati unahofu na wasiwasi juu ya maisha yako, unajiuliza likitokea tatizo itakuaje? Au hitaji fulani linalokuja hivi karibuni litakuwaje? n.k.Unapokuwa na fungu fulani la akiba huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani unajua hata ukikosa fedha akiba yako itakusaidia.
 
Hukuwezesha kuandaa kesho vyema

Maandalizi ya kesho yanafanywa leo. Kuweka akiba maana yake unajiandaa kwa mahitaji ya kifedha ya baadaye — yaani kesho. Mtu asiyeweka akiba mara nyingi hafikiri kuhusu kesho wala hana malengo kwa ajili ya baadaye yake.Ili kujenga baadaye au kesho njema, ni muhimu pia kuimarisha msingi wako wa kiuchumi kwa njia ya kuweka akiba.
 
Hukuwezesha kuwahi fursa

Ni mara ngapi umekuwa ukisema au ukisikia kauli kama vile “Ningekuwa na pesa ningenunua hiki kitu”, “Ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye hii huduma”, “Ningekuwa na pesa ningejiunga na huu mradi”, n.k.Hili linadhihirisha kuwa watu hukosa fursa mbalimbali kutokana na kukosa akiba ya fedha. Unapokuwa na akiba ya fedha ni rahisi kuwahi fursa mpya au bidhaa zenye manufaa mara zinapopatikana.
 
Hitimisho

Fedha ni jambo linalohitaji nidhamu na busara ya hali ya juu; vivyo hivyo kuweka akiba ni swala linalohitaji kufanya maamuzi sahihi ili uweze kulitekeleza.Baada ya kusoma makala hii, naamini sasa hutopuuza tena swala la kuweka akiba. Hakikisha hutumii akiba yako pasipokuwa na sababu ya msingi; tambua itakusaidia sana mbeleni wakati wa uhitaji.Je wewe huwa unaweka akiba? Je unanufaika vipi kwa akiba yako?
 
Kumeshuhudiwa watu wakiishi maisha ya taabu na mahangaiko makubwa baada ya kustaafu. Hili linatokana na kutokujiandaa vyema kabla ya kustaafu.Kwa kufahamu umuhimu wa kujiandaa vyema kabla ya kustaafu; karibu ufahamu mambo 6 muhimu ya kufanya kabla ya kustaafu.
 
Jiandae kisaikolojia

Kustaafu ni kipindi tofauti sana na kipindi ulichokuwa kwenye ajira. Kipindi hiki utakutana na mtindo mpya wamaisha tofauti na ule uliouzoea.Ni muhimu kujiandaa kisaikolojia kwa maswala kama vile kukaa bila kupata mshahara, ofisi, gari la kampuni au taasisi, nyumba ya taasisi au kampuni pamoja na manufaa mengine ya wafanyakazi.Andaa fikra zako kutambua kuwa wakati wa kufaidi mambo mbalimbali kutokana na kazi yako sasa umefikia mwisho.
 
Weka akiba

Ikiwa kazi yako ndiyo uliyokuwa unaitegemea kama chanzo chako cha kipato, basi tafakari juu ya maisha bila kazi hiyo. Hakikisha unaweka akiba ya kutosha itakayokuwezesha kumudu matumizi yako mbalimbali baada ya kustaafu.Unaweza kuweka akiba ya pesa au ya vitu ambavyo vinaweza kubadilishwa kuwa pesa kama vile ardhi, mifugo au majengo.
 
Lipa madeni

Kumbuka baada ya kustaafu kiwango chako cha kipato kitapungua; hivyo ni muhimu kulipa madeni kabla ya kustaafu ili usije ukahangaishwa na madeni wakati wa kustaafu.Ikiwa una mkopo au deni la mtu binafsi, basi hakikisha unafanya juu chini ili ulilipe kabla ya kustaafu.
 
Ondoa matumizi yasiyo ya lazima

Kama nilivyotangulia kueleza kwenye hoja zilizotangulia, baada ya kustaafu kiwango chako cha mapato kitapungua.Hivyo ni muhimu kutazama upya matumizi yako. Hakikisha matumizi yote ambayo hayana umuhimu au ulazima unayaepuka.Unaweza kuzingatia haya:Epuka manunuzi makubwa sana. Ikiwa unapanga kununua vitu kama vile gari, nyumba au kiwanja bada ya kustaafu, tafakari vyema suala hilo.Epuka huduma ambazo siyo za lazima.Weka utaratibu mzuri wa kutunza wanaokutegemea. Ikiwa una watoto ambao bado wanasoma au ndugu wanaokutegemea, basi weka mikakati stahiki ya kuwatunza.
 
Tafuta chanzo kingine cha pesa

Kwa kuwa ulikuwa unategemea kazi yako kama chanzo chako cha kipato, ni muhimu sana kutafuta chanzo kingine cha kipato. Usisubiri hadi ustaafu ndipo upate chanzo kingine bali anza kutafuta chanzo hicho kabla hujastaafu.Nimeshuhudia watu wengi wakianzisha biashara baada ya kustaafu lakini wengi huishia kufilisika kutokana na kukosa uzoefu. Ni muhimu ukaanza mapema ili ujijengee uzoefu.
 
Jiunge kwenye bima ya afya

Mara baada ya kustaafu utahitaji huduma za afya hasa kutokana na matatizo mbalimbali ya uzeeni. Unapokuwa umejiunga na bima ya afya utaweza kupata matibabu kwa urahisi na kwa gharama nafuu.Unaweza pia kuwaunganisha wanafamilia wako ili wasikuwekee mzigo mkubwa wa gharama za matibabu. Kwa kufanya hivi utapunguza gharama za matibabu mara baada ya kustaafu.
 
Kwa hakika maandalizi mazuri ya kesho hufanywa leo. Ni muhimu kujiandaa kwa kipindi cha kustaafu mapema ili usihangaike wakati utakapostaafu. Kumbuka baada ya kustaafu hutoweza kufanya kazi kwa nguvu tena kama zamani kwani hata nguvu ya mwili imepungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…