Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Everything in life is temporary.

Just because life isn't easy at the moment,
doesn't mean you can't laugh.

Just because something is bothering you,
doesn't mean you can't smile.

Every moment gives you a new beginnning
and a new ending.

You get a second chance every secon.

You just have to take it and make the best of it.

Nothing lasts forever.
.
.
 
JINSI YA KUPIKA MAHARAGE KWA KUTUMIA CHUPA YA CHAI

Kuna njia mbali mbali za kupika maharage lakini kuna moja haitambuliki sana na watu wengi ingawa inahitajika mpishi awe na subira pale anapotumia mbinu hiyo.

Unachohitaji kuwa nacho ni Chupa ya chai au Thermos Flask pekee na utapika maharage mpaka yaive kwa njia nyepesi na bora zaidi.

JINSI YA KUPIKA

1. Kwanza, tafuta chupa ya chai (Thermos Flask) ambayo itakuwa na ukubwa sawa na maharage unayotaka kupika.

2. Pima kiwango cha maharage unachohitaji kwa kutumia kikombe.

3. Chemsha maharage hayo kwa muda mfupi kwenye sufuria.

4. Kisha yaweke kwenye chupa yako ya chai

5. Yaache kwa muda wa masaa sita kama ni usiku yaache yalale ndani ya chupa hiyo.

6. Baada ya hapo, maharage yako yatakuwa yanafaa kupikwa vizuri kwa viungo (Kuungwa) kwa ajili ya Kuliwa

NB ; NI NJIA ZURI JAPO WENGI HATUNA MAZOEA NA PIA INA SAVE SANA GHARAMA YA MKAA
 
JINSI YA KUPIKA UBUYU
MAHITAJI

1. Sukari vikombe 2
2. Maji vikombe 2
3. Nusu kikombe unga wa ubuyu
4. Vikombe 4 ubuyu wenyewe
5. ¼ Kijiko cha pili pili ya unga
6. ¼ Kijiko cha chumvi
7. ¼ Kijiko cha iliki ya unga
8. Rangi nyekundu au yeyote utakavyopenda. ️JINSI YA KUTENGENEZA

1. Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.
2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito.

Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu.
3. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.
4. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu.
5. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.
 
JINSI YA KUPIKA KABABU ZA NYAMA YA KUSAGA
MAHITAJI
1. Nyama ya kusaga Kilo 1
2. Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa Kijiko 1 cha chai
3. Pilipili mbichi iliyosagwa kijiko 1 cha chai
4. Bizari ya Kababu ½ paketi
5. Chumvi kiasi
6. Mafuta kiasi ya kukaangia ️
7. Mayai 2
8. Slice 2 za mkate

JINSI YA KUPIKA
1. Weka nyama Yako katika bakuli kubwa

2. loweka slice za mkate katika maji kisha zikamue maji uzivuruge kwa mkono ndani ya nyama hakikisha zinachanganyika na nyama vizuri

3. Changanya nyama pamoja na viungo vyote katika bakuli.

4. Chukuwa mayai yako vunjia katika huo mchanganyiko changanya tena mpaka vichanganyike

5. Fanya madonge shape ya duara kama kwenye picha weka kando.

6. Kisha Kaanga kama sambusa mpaka Zibadilike rangi.

7. Epua zikiwa tayari kwa kuliwa.
 
JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI ️MAHITAJI

1. Njegere nusu kilo

2. Nazi 2

3. Nyanya 4

4. Karoti 1

5. Pilipili hoho 1

6. Kitunguu maji 1

7. Thoum kiasi

8. Mafuta ya kupikia kiasi

9. Chumvi kiasi ️

JINSI YA KUPIKA NJEGERE

1. Chambua njegere, zikoshe, kisha zitie kwenye sufuria na maji uzichemshe ziive kiasi lakini zisilainike sana.

2. Safisha nyanya uzimenye na kuzikata. Pia katakata hoho, karoti na vitunguu. Twanga vitunguu thoum. kisha kuna nazi uchuje tui zito na jepesi.

2. Bandika sufuria jikoni, weka mafuta ukaange vitunguu, vikishabadilika rangi tia hoho kaanga kidogo kisha utie thoum na nyanya pamoja na karoti, endelea kukaanga.

3. Mimina njegere, tia chumvi na umimine tui jepesi, wacha lichemke. kisha tia tui zito liache lichemke kiasi na uzito wa njegere ukiwa sawa, tayari epua.
 
JINSI YA KUPIKA DOUGHNUT ️MAHITAJI

1. Unga wa ngano kilo 1

2. Mafuta ya kupikia lita 1

3. Sukari ilosagwa robo kilo

4. Siagi
5. Maziwa robo lita

7. Mdalasini ulosagwa
8. Mayai 3
9. Baking powder kijiko 1 kikubwa
10. Hamira

JINSI YA KUPIKA DONAT

1. Changanya unga na baking powder pamoja na siagi hadi unga uchanganyike tia sukari kidogo, kungumanga na yai kisha endelea kuchanganya unga.
2. Weka maziwa na kanda mpaka upate donge laini tengeneza madonge, uanze kusukuma unga kiasi cha sentimeta moja. Usiwe mwembamba sana kama wa chapati.

3. Kata duara kwa glasi au kikombe kisha kata duara lingine dogo katikati kwa kutumia kifuniko cha chupa ya maji au kitu chochote chenye duara dogo, upate shepu ya ringi.

4. Bandika mafuta jikoni, yakipata moto tia donats uzikaange mpaka ziwe na rangi nzuri ndipo uzitoe.
 
JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA MAJI ♦️MAHITAJI

1. Ngano ½ kilo

2. Mayai 3

3. Mafuta ¼ kikombe
kitunguu kikubwa kilichosagwa 1

4. Kitunguu Swaumu punje 4

5. Chumvi ½ kijiko au zaidi kulingana na matakwa yako ️
♦JINSI YA KUPIKA CHAPATI

1. Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi.

2. Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito sana wala si mwepesi sana.

3. Ongeza mayai na chumvi endelea kukoroga.

4. Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto.

5. Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili.

6. Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka iwe rangi ya kahawia.

7. Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia.
 
JINSI YA KUPIKA ROST LA NYAMA YA NG'OMBE
MAHITAJI
1. Nyama nusu
2. Nyanya 3 kubwa
3. Tomato paste kijiko 1
4. Kitunguu/swaumu
5. Hoho
6. Karoti
7. Pilipili
8. Mafuta ya kupikia
JINSI YA KUPIKA ROST
1. Chemsha nyama adi iive Weka sufulia jikon weka mafuta ya kupikia
2. Weka kitunguu weka swaumu tia nyama
3. Geuza weka tomato paste
4. geuza Weka nyanya funika adi ziive tia hoho na karoti na pili pill weka mchuz unaotaka weka chumvi funika.
 
Mkataba wa David Silva mwenye umri wa miaka 34, kwa Manchester City unakamilika Juni 30 lakini Mhispania huyo anayecheza safu ya kati,yuko tayari kuongeza mkataba huo hadi mwisho wa msimu, kabla ya kufunganya virago. (Times - subscription required)
 
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 31, has amaemshauri mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland,19 - ambaye anang'ang'aniwa na Manchester United na Real Madrid - kuendelea na ukuzaji wa talanta yake Borussia Dortmund. (Metro)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…