D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
[Kuwa huo unaoitwa mpango] ulioasisiwa na mmoja wa viongozi wakuu wa kisiasa wa mapinduzi ya 1964 (Babu) ukijumuisha viongozi wa kijeshi wa mapinduzi ya kutumia silaha ya 1964, pamoja na Mkuu wa Uendeshaji wa Jeshi la Tanzania (Mahfoudh) na kuandaliwa kwa makini katika kipindi cha zaidi ya miaka minne ulikuwa ni kumpeleka mtu mmoja, (Ahmada) kuiteka kambi ya Bavuai, Makao Makuu ya Jeshi na Chuo cha Radio cha Jeshi, mtu mmoja (Dugheshi) kumkamata Karume, kumpeleka kwenye stesheni ya radio na … [ baadae] … Kuiteka Ikulu … Mtu mmoja (Baramia) kuyadhibiti Makao Makuu ya Umoja wa Vijana, ambayo ni kituo kilichokuwa cha kijeshi chini ya kiongozi mkuu wa usalama wa ndani wa Karume, Seif Bakari, na bila shaka kuwepo mtu mmoja wa akiba (Ameir) ili kushughulikia shambulizi lolote la upinzani … washitakiwa wengi ambao walituhumiwa kupangiwa majukumu ya kijeshi hawakuwa wanajeshi katika jeshi la Zanzibar. (Chase, 1976: 29)
Adhabu za kifo 42 zilitolewa na Mahakama ya Wananchi. Kumi na tatu ya hukumu hizo zilitolewa wenyewe wakiwa hawapo, kwa watu ambao waliowekwa kizuizini bara lakini hawakukabidhiwa kwa serikali ya Zanzibar ikitiliwa maanani kuwa washtakiwa hao wasingelifanyiwa kesi ya haki. (Amnesty International, 1979: 1)
Mwezi mmoja baada ya kesi iliyofanyika katika mahakama ya bandia nchini Zanzibar kumalizika na hukumu kutolewa, tulihamishiwa katika magereza mengine. Baadhi yetu, Salim Saleh, Shaaban na Badru Said, Haji Othman na mimi mwenyewe, tulihamishiwa Dodoma; Ahmed Tony na Tahir Ali walipelekwa Tabora na Amour Dugheish na Abdalla Juma walipelekwa Mbeya; Suleiman Sisi alipelekwa Mwanza na Hashil alipelekwa Tanga. Babu na Ali Mahfoudh walibakia Ukonga kwa muda wote. Ali Yusuf aliachiliwa miezi michache baada ya kesi. (Mahojiano na Hamed Hilal, 2011)
Tarehe 30 Machi, 1978, Aboud Jumbe alizifuta tatu katika jumla ya hukumu za kifo, zilizotolewa kwa washtakiwa, na tarehe 26 April, 1978, wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 13 ya Muungano, hatimaye Nyerere aliamuru kuachiwa kwa Babu na wengine kumi na mbili waliokuwa kizuizini bara. Ijapokuwa wote waliokuwa kizuizini bara waliachiliwa, hukumu za kifo kwa wanne wao – Babu, Ali Mahfoudh, Tahir Ali Salim na Hamed Hilal – kamwe hazikufutwa.Habusu kimekuwa ni chombo muhimu cha mapambano. Litakuwa muhimu sana kama mungeliweza kulitoa kwa uchache kila mwezi. Hivi sasa hiyo ni silaha pekee inayoweza kutuletea ukombozi wetu. Lina uwezo wa kuwa kama ‘jukwaa’ maarufu kwa ajili ya ‘ujenzi wa nyumba’. Tafadhali hakikisheni kuwa nakala nyingi iwezekanavyo zinafika Tanzania, hasa Zanzibar.[1]