Mapema mwaka 1955, Reeves alisaini mkataba wa miaka 10 na Kampuni ya RCA Victor chini ya Steve Sholes, ambaye alitoa rekodi za kwanza za Reeves akitumia Kampuni ya RCA na pia akaingia mkataba na Elvis Presley na kampuni hiyo hiyo mwaka huo huo.
Alipokuwa akirekodi mwanzoni akiwa na Kampuni ya RCA, Reeves bado alikuwa anaimba kwa staili ya sauti ya juu ambapo ilionekana ndio kipimo cha nyimbo za ‘Country’ Wanamuziki wa Magharibi kwa wakati huo.
Baadaye Jim alianza kupunguza sauti yake wakati akiimba na kutumia ‘Pitch’ ya chini akiimba huku midomo yake ikikaribia kugusa kipaza sauti, ingawaje waliokuwa wanamrekodi (RCA) walikuwa wanailalamikia hali hiyo.
Mwaka 1957 kwa maelekezo ya ‘Produysa’ wake Chet Arkins alitumia mtindo huo katika toleo la wimbo wa maonesho wa ‘Penzi lililopotea’ uliokusudiwa uimbwe na mwimbaji wa kike.
Katika kipindi chote miaka yote ya 1950 na hadi 1960 mwanzoni, Jim Reeves aliachia nyimbo zake kali zizoshika ‘chati’ za ‘Anna Marie’ na ‘Blue Boy’ No. 2 za mwaka 1958.
Alifyatua kibao kingine cha ‘Billy Bayo’ mwaka 1959 na ‘He will have to go’ wa mwaka 1960., ‘Adious Amigo’ (namba mbili, 1962), ‘Welcome to my World’ (namba mbili, 1964) na ‘I guess I’m crazy’ (namba moja kwa wiki saba, 1964).
Wimbo wake, ‘Danny Boy’ akijitambulisha kwamba wazazi wake wametokea Irish. Wimbo ‘But You Love Me Daddy’ ukirekodiwa wakati mmoja akiwepo ‘Steve’ mtoto wa miaka minane wa mpiga gitaa la besi, Bob Moore, ulikuwa katika ishirini bora huko Ulaya miaka kumi Baadaye.
Rekodi zake mara nyingi zilikuwa na utamanifu wa kipekee, kama ‘I Love you Because’ (ulishika namba 5) na ‘I won’t forget You’ (namba 3) zilikuwa katika chati huko UK kwa wiki 39 na 25 mfululizo.
Reeves alikuwa amesaidia sana kuanzisha staili mpya ya muziki wa ‘Country’ akitumia ‘violin’ na ‘mpangilio wa kupendeza wa background ikijulikana kama ‘Nashville’ sound.
Hali kadhalika Jim Reeves amekuwa hodari kwa kuukweza na kuzipa maarufu nyimbo nyingi za ‘Injili’ kama ‘We Thank Thee’ ‘Take My Hand, Precious Lord’ ‘Across The Bridge’ ‘Where We’ll Never Grow Old’ na nyingine nyingi.
Kwa kweli kulikuwa na mafanikio makubwa kwa muziki huu wa kawaida na wa ‘Country’ ambapo ulimpatia ‘Platinum Record’ ambayo ilitolewa mwishoni mwa mwaka 1959 na ilifanikiwa kuwa namba moja katika gazeti la ‘Billboard’.
Mwana historia wa muziki wa Country, Bill Malone alionesha kwamba ni katika namna nyingi Reeves aliendeleza utamu na ubora katika muziki wa ‘Country’ kimpangilio na ‘melodi’ safi na ujumbe unaogusa mioyo ya watu.
Kwa nyongeza, Malone alimsifia Reeves kwa staili yake ya kuimba ambayo anaishusha chini sauti yake, inakuwa kama ya kubembeleza na ndio maana watu wengi wanatamka kwamba Jim Reeves ni muimbaji mwenye sauti ya mguso.