Kwa nyongeza, Malone alimsifia Reeves kwa staili yake ya kuimba ambayo anaishusha chini sauti yake, inakuwa kama ya kubembeleza na ndio maana watu wengi wanatamka kwamba Jim Reeves ni muimbaji mwenye sauti ya mguso.
July 31, 1964, Reeves na mshirika mwenzake wa kibiashara, Meneja Dean Manuel waliondoka Batesville, Arkansas kupitia Nashville wakitumia ndege ya injini moja akiwa Reeves anaendesha.
Baada ya masaa 42 mabaki ya ndege yalionekana ikiwa mbele, yaani usoni pamoja na injini vimejikita ardhini. Reeves na mwenzake walikutwa tayari wamekwisha fariki.
Mjane wake, Mary Reeves (70) alifariki katika siku ya ‘Veteran’ Tarehe Novemba 11, 1999, iliripotiwa kuwa amekufa akiwa peke yake katika nyumba ya kuuguza wagonjwa.
Kutokana na Mary Reeves Davis kushindwa kutokana na ugonjwa kuzisimamia mali za Jim Reeves ziliuzwa kwa ‘United Show of America’ mwaka 1997 kwa thamani ya Dola za Kimarekani milioni 7.3