Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati huo huo, bosi wa RB Leipzig, Oliver Mintzlaff amesema kwamba dili la Werner kwenda Chelsea bado halijamilika, akisema: “Bado hatujamalizana na Chelsea. Hivyo, kwa sasa Timo Werner bado hakuna kilicholipwa kuvunja mkataba wake, wala klabu kutuma maombi ya kutaka kumsajili.”
 
Kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, 32, anataka kusalia katika klabu ya Barcelona hadi pale kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu wa 2021 licha ya ripoti kusema kwamba ataondoka mapema. (Goal)
 
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Chelsea Michael Ballack ameunga mkono uamuzi wa kumsaini mshambuliaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24 Timo Werner kutoka klabu ya RB Leipzig na anaamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ataizoea rahisi ligi ya premia.. (Sky Germany)
 
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Ander Herrera, 30, anasema kwamba mchezaji mwenza wa Uruguay Edinson Cavani, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu anataka kucheza nchini Uhispania. Mshambuliaji Cavani mwenye umri wa miaka 33 amehusishwa na uhamisho wa kuichezea Atletico Madrid. (Diario As via Mail)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…