Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umati wa mashabiki wa Liverpool jana ulilazimika kuvunja masharti na miongozo ya kujikinga na Virusi vya Corona kwa kuamua kuingia mitaani katika maeneo tofauti ya Uingereza ili kusherehekea ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu ambao timu yao imeupata jana
 
Baada ya kusubiri kwa miaka 30, Liverpool jana walitawazwa rasmi kuwa mabingwa kufuatia kipigo cha mabao 2-1 ambacho Manchester City walikipata kutoka kwa Chelsea katika mechi iliyochezwa usiku kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
 
Licha ya kuwepo kwa katazo la mikusanyiko ili kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona, kwa siku ya juzi mashabiki wa Liverpool waliamua kwenda kinyume na katazo hilo na kuamua kuburudika kutokana na furaha waliyokuwa nayo kwa ubingwa huo.
 
Kutimizwa kwa kiu ya mashabiki hao ya kutwaa taji la kwanza baada ya kusubiri kwa miaka 30 tangu walipotwaa kwa mara ya mwisho msimu wa 1989/1990, kulionekana kuwasahaulisha mashabiki hao na kukiuka masharti na miongozo ya kujikinga na virusi vya Corona ambayo imewekwa na serikali ya Uingereza.
 
Wachezaji wa Liver nao walionekana kushangilia kwa nguvu ubingwa huo wakiwa wameketi pamoja wanaifuatilia mechi hiyo kwenye runinga na baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa walinyanyuka kwenye viti na kuanza kurukaruka huku wakipongezana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…