Vifo vinne vilivyotokea wakati wa utafiti huo, hakuna ambaye alikuwa na umri wa chini ya miaka 10 na wawili kati ya hao waliokufa walikuwa na matatizo mengine ya kiafya.
Zaidi ya nusu ya watoto walioshirikishwa kwenye utafiti walilazwa hospitali na asilimia 8 wakahitajika kupata huduma kutoka chumba cha wagonjwa mahututi.
Asilimia 65 ya watoto hao walionesha homa, asilimia 54 walikuwa na maambukizi upande wa juu wa njia ya upumuaji, asilimia 25 walikuwa na ugonjwa wa nimonia na asilimia 22 wakawa na dalili za matatizo ya utumbo
Asilimia 16 ya watoto ambao wengi wao walipimwa kwasababu ya kuwa karibu na watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona, hawakuwa na dalili zozote kabisa
Watafiti wanasema kiwango cha vifo kwa watoto kuna uwezekano mkubwa kikawa chini kuliko kile kilichojitokeza kwenye utafiti huo kwasababu hadi wakati huo, walio na dalili za wastani huenda hawakuwa wamepimwa au kubainika.
Hatahivyo, data zaidi inahitajika kusaidia madaktari kufanya maamuzi ya machaguo ya tiba stahiki kwa watoto ambao wanauguwa kwasababu ya virusi vya corona, akaongezea.