Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
________
Watu wanasema mengi kuhusu kilichotokea Malawi. Kwenye chaguzi, wanajimu, waganga, wachambuzi na manabii ni wengi. Nami natupia "uzushi" wangu kwa maeneo matatu:

1. Kilichotokea Malawi ni maasi: Alianza Rais Mutharika akawaasi wapiga kura. Wakafuata wananchi; wakaasi mamlaka. Likafuata jeshi, likaasi mamlaka na kutii waasi (wananchi). Lakini Uasi wote ulianza kwa viongozi; wananchi wakaiga kutoka kwa viongozi. Maasi yanayoanzia kwa viongozi hufanikiwa. Maasi yasiyoanzia kwa viongozi ni vigumu kufanikiwa. Chunguza historia.

2. Waafrika wanachukia kubezwa.
Kumpa mtu chakula kisha ukamsema hadharani anachukia sana. Maendeleo yanapendeza yakijitangaza kuliko kuyatangaza. Watendewa wana macho na midomo. Waache waseme wenyewe kuliko wewe kuwasemea.

3. Maendeleo bila haki ni ibada ya sanamu. Haki bila maendeleo ni dawa ya maumivu isiyotibu ugonjwa. Hekima ni kuweka mizani katika hayo mawili.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…