Alikuwa na miaka kumi na mbili tu alipoanza kutembelea Nyumbani kwa yule aliyemuita Mjomba, ama Anko kama alivyopendelea kuitwa.Alifika pale mara nyingi kwa ajili ya kucheza na rafiki yake umri sawa na yeye.
Siku moja alipofika kwa ajili ya kucheza na rafiki yake hakumkuta...
Ni anko pekee aliyekuwepo Nyumbani, aliaga ili aondoke lakini anko huyu alimsihi sana amsubiri rafiki yake kwani yu njiani anarejea na punde angeliwasili.