Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vilevile kazi wanazofanya zinatofautiana ikiwamo wapo wanaotumia muda mwingi kuinama, kukaa au kusimama. Makundi yote haya yanaweza kuwa katika hatari ya kupata matatizo ya mgongo endapo watafanya kwa muda mrefu.
 
Maumivu ya mgongo ni moja ya matatizo ya kiafya yanayojitokeza mara kwa mara na huathiri zaidi misuli na mifupa ya mgongo. Tatizo hili linawaathiri karibu asilimia 40 katika moja ya hatua za maisha yao.
 
Maumivu ya mgongo yapo ya kawaida; chini ya wiki 6, yapo ya kati; wiki 6 hadi 12 na maumivu sugu; ambayo yanadumu kwa zaidi ya wiki 12. Maumivu haya yakianishwa zaidi yanaweza kutokana na kupata majeraha ya kawaida au mambo yasiyo ya majeraha na chanzo maumivu hayo kinaweza kuwa eneo husika au maumivu yalitokea mahali pengine mwilini.
 
Mara nyingi maumivu haya chanzo na sababu hasa hakigunduliki moja kwa moja na hakujitokezi mapema, lakini inaaminika kuwa chanzo cha maumivu haya huenda yametokana na kujeruhiwa kwa misuli au mifupa ya mgongo.
 
Endapo itatokea maumivu hayo kutoisha baada ya matibabu ya kawaida ama kuambatana na viashiria hatari kama vile kupungua uzito kusikokuwa na sababu maalumu, homa kali, kushindwa kuhisi chochote maeneo ya makalio au miguu na kushindwa kujongea vizuri, hali kama hizi lazima hatua za haraka zitahitajika kwa ajili ya uchunguzi kwani ni kawaida maumivu ya mgongo kupotea baada ya matibabu chini ya wiki sita kwa asilimia 40-90 ya wagonjwa.
 
Umbile la mgongo ni kama vile herufi S likiwa na maeneo makuu manne, yaani cervical, thoracic, lumber, sacral na coxgeal. Mgongo unaundwa na pingili za vifupa 24 vilishikizwa na kutengeneza maungio. Pia kuna vifupa tisa vilivyoshikamana katika muishilio wake.
 
Pia kuna vifupa tisa vilivyoshikamana katika muishilio wake. Hivi ndivyo vinaonekana kama mkia na kufanya jumla ya mifupa 33. Katikati ya pingili hizi huwa na kitu kama santuri inayofanana na plastiki, pia huwa na matundu ya pembeni na kati, na kutengeneza mfereji maalumu unaopita uti wa mgongo.
 
Kifupa cha kwanza na cha pili ndivyo vinavyoweza kufanya mijongeo mbalimbali kama vile inayoashiria ndio na hapana kwa mwitiko wa kichwa. Vilevile mifupa 12 ya mbavu hukutana na pingili za mifupa ya mgongo na kutengeneza ungio.
 
Vilevile mwishilio wa mgongo ndio kwa kiasi kikubwa unasaidia kutembea. Maumivu ya mgongo hujitokeza zaidi kwa watu wa umri wa miaka 20 hadi 40. Baadaye nusu ya wagonjwa hupata maumivu makali kuliko ilivyokuwa mwanzoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…