Inaaminika kuwa ukiwa na Madimpo' husaidia kukufanya kuonekana mdogo zaidi kuliko umri wako. Lakini kumbuka uwepo wa Madimpo' ni kutokana na matatizo ya Jenetikia (Genetics).
Ulimi wa Twiga' una rangi ya bluu, Kutokana na kutumia zaidi ya saa 12 kula matawi mbalimbali juu ya miti hivyo husaidia Ulimi' wake kutokuungua na Jua pindi anapofanya kitendo hicho kwa muda mrefu.
Kama upo chini ya miaka 38 bado, Takwimu zinaonesha kichekesho ambacho kitakufurahisha zaidi ni kile ambacho hujawahi kukisikia kabisa katika maisha yako.
Kama huna Dimpo' kuna mashine maalum za kutengeneza madimpo, Unavaa kifaa maalum usoni ambacho huanza kuchonga madimpo' kwenye mashavu yako. Mashine ya kwanza ya kutengeneza Madimpo' iliundwa mwaka 1936 na Isabella Gilbert.
Samsung kupitia bidhaa ya simu, wanapata pesa nyingi zaidi kutokana na biashara wanayofanya na Apple (Iphone) kuliko mauzo ya simu wanazozalisha wenyewe.
Kwa mujibu ya wataalam wa lugha, Neno "Huh?" Lina maana sawa haijalishi limetamkwa kwenye lugha gani yoyote ile, iwe Kiingereza, Kiswahili, Kichina au etc
Kwa mujibu wa World Economic Forum, Mpaka kufikia mwaka 2025, Nusu ya waajiriwa duniani itawabidi kuboresha zaidi ujuzi wao ili kuepukana na tatizo la ukosefu wa ajira ambao utachangiwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Sababu mojawapo zinazopelekea baadhi ya wanyama kuua watoto wao ni Upungufu wa chakula na zaidi Majike' mfano Simba na Nguruwe humla mtoto kama atagundua ni mgonjwa lengo ni kuondoa hatari kabisa kutoka kwa wanyama wengine hatarishi kama Fisi.