Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hawa hapa ndiyo wanyama 10 wenye akili zaidi duniani.TemboTembo wana akili kubwa kuliko mnyama yeyote wa ardhi kavu, tembo ana uwezo wa kutafuna majani ya dawa kuanzisha uchungu wa kuzaa, kutambua vitu kwenye kioo, kuigiza sauti mbalimbali na kutumia vitu mbalimbali kwa matumizi sahihi pasipo kufundishwa, pia ndiyo wanyama pekee wanaoweka msiba pale mwenzao anapokufa.
 
Pweza

Ana uwezo wa kutoroka akikamatwa na kufungiwa kwenye mzingile (maze) ana ubongo mkubwa kuliko wanyama wote wasio na uti wa mgongo lakini pia wana uwezo mkubwa wa kujua maadui, ndio mnyama pekee wa kundi hilo kutumia zana, hujibadili kukwepa maadui, mfano mzuri ni Pweza Paulo aliyetabiri Hispania kuchukua kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.
 
Njiwa

Ana uwezo wa kutambua herufi zote 26, ana uwezo wa kurudi nyumbani hata akiwa kilomita mia kutoka nyumbani na ndiyo sababu walikuwa wanatumika kutuma ujumbe kwa wauza madawa ya kulevya pia wanatumika kuuza madawa hasa magerezani.
 
Mbwa

Ni marafiki wakubwa wa binadamu, ambapo mbwa wa kawaida ana akili sawa na mtoto wa binadamu mwenye umri wa miaka miwili, wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu, kujilinda, na kujifunza kutoka kwa binadamu.
 
Nguruwe

Wanatunza kumbukumbu kwa muda mrefu, wana uwezo wa kuwasiliana na wenzake na ndiyo mnyama msafi zaidi katika wanyama wanaofugwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…