Mwanamama wa makamo alimpatia mwanamke raia wa Costa Rica (46) kiasi cha dola 175 za Marekani ili aolewe na Mwanaume wa kichina ili aweze kupata makazi kwenye eneo zuri
Mwanamama wa makamo alimpatia mwanamke raia wa Costa Rica (46) kiasi cha dola 175 za Marekani ili aolewe na Mwanaume wa kichina ili aweze kupata makazi kwenye eneo zuri
Katika eneo analoishi usalama ni mdogo.''maeneo haya namna ambavyo hutakuwa na habari nyingi ndivyo utakavyoishi kwa muda mrefu.'' mkazi wa eneo hilo alitahadharisha
Kilichotokea kwa Maria si jambo geni hapa. Mwanasheria au mtu wa kati hufika kuwatafuta watu wenye shida na pesa na kuwashawishi kuolewa na raia wa kigeni ambao hata hawajawahi kukutana.
Maria aliolewa bila hata kuyaacha makazi yake.Aliingia ndani ya gari kisha akaweka saini vyeti vya ndoa na kupata dola 175 kwa makubaliano kuwa akiolewa baadaye atapewa talaka mapema iwezekanavyo.
Amesema mtandao huo unafanya kazi kwa namna mbalimbali , wengine wakienda mbali zaidi kwa kuiba vitambulisho na kuwaozesha kwa raia wa kigeni ili kupata makazi pia uraia kupitia ndoa hizo.