Wengine ambao waliingia kwenye ndoa bandia ili kujipatia pesa walijikuta wakiishi na ndoa hizo kinyume cha makubaliano kuwa wangefanya mchakato wa kupata talaka, wanawake wameendelea kutambulika kwa wanandoa na wanaume wasiowafahamu na hata kufahamu wapi pa kuwapata.
Kuns Nyaraka tulizoona zinasema raia mmoja wa China ambaye alikuwa hazungumzi lugha ya spanish, alitia saini nyaraka ambazo alifikiri ni za maombi ya makazi, kumbe zilikuwa nyaraka za cheti cha ndoa.
Sheria kali ya uhamiaji ilianzishwa mwaka 2010 ilisaidia kupambana na tatizo hilo, wanaohusika na upangaji wa ndoa feki uhukumiwa kifungo cha mpaka miaka mitano gerezani
Raia wa kigeni bado wanaweza kuomba kibali baada ya kufunga ndoa na mwenza raia wa Costa Rica wakiwa na vyeti vya ndoa vilivyosajiliwa, lakini vibali hutolewa kwa mwaka mmoja tu, ambapo mwombaji atapaswa kuomba tena kila baada ya mwaka.