Mwaka 2018 wakala wa Yaya Toure alisema kua"Miungu ya kiafrika haitamuacha Guardiola ashinde CL miaka ijayo hii Itakua Kama laana ya kiafrika nawaambieni mda tu ndo utaongea kama nipo sahihi au laa" Leo guardiola kapoteza fainali ya UEFA dhidi ya Chelsea naona Kama laana ya kiafrika imemshukia...
Manchester United wanamfuatilia mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo huku klabu hiyo ya Italia ikiwa iko tayari kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa miaka 36 kwa kubadilishana na kiungo wa kati Paul Pogba , 28. (Gazzetta dello Sport via Express)
Tottenham wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus,24, ambapo itashuhudia kubadilishana na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane,27, pamoja na nyongeza ya fedha.(Star)
Kiungo wa kati Dani Ceballos, 24, amesema anataka kusalia Real Madrid msimu ujao au kuondoka kabisa kwenye klabu baada ya kutumia misimu miwili akichezea klabu ya Arsenal (Mail)
Kocha wa zamani wa England ma Crystal Palace yuko kwenye orodha ya kuchukua nafasi ya ukufunzi kwenye klabu ya West Brom baada ya kuondoka kwa Sam Allardyce. (Mirror)
Tottehnam wana mpango wa kuanza mazungumzo rasmi na Paris St-Germain siku ya Jumatatu ukiwa mpango wa kumrejesha Mauricio Pochettino kwenye klabu. (Sun)
Mshambuliaji wa Tottenham Steven Bergwijn anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu wa joto huku Ajax ikiwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo, 23.(De Telegraaf
Aston villa wana hofu ya kumpoteza kiungo wao nyota Douglas Luiz ,23, huku timu yake ya zamani ya Manchester City ikihitaji kumsajili tena Mbrazili huyo.(90 Min)
West Ham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Mzambia Patson Daka wanapotafuta namna ya kuziba nafasi ya Sebastian Haller. Mchezaji huyo wa miaka 22 pia amevutiwa na Liverpool, Manchester United na Manchester City. (Zam Foot)