Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Moja ya viinilishe viwili mhimu zaidi katika kufanya kazi hiyo ni hivi vijulikanavyo kama Lutein na Zeaxanthin vipatikanavyo katika mayai, ambavyo ni viuaji sumu vyenye nguvu au vyenye kazi ya kuondoa sumu ambavyo hujijenga katika retina ya jicho.
 
Tafiti zinasema matumizi ya kutosha ya viinilishe hivi viwili yanaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kupatwa na ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataract).Kwa ujumla kiini cha yai kina kiasi kingi kabisa cha Lutein na Zeaxanthin.
 
Mayai yana protini yenye ubora wa hali ya juu na amino asidi mhimu kwa uwiano mzuriProtini ndiyo matofali mhimu zaidi katika ujenzi wa mwili wa binadamu.Protini hutumika kutengeneza aina zote za tishu na molekuli ambazo ni mhimu katika ujenzi na ufanyaji kazi wa mwili.
 
Kupata kiasi cha kutosha cha protini katika mlo wako ni mhimu sana na tafiti zinaonyesha kiasi cha protini ambacho kimependekezwa kuwa ndicho unachopaswa kula kila siku chaweza kuwa ni kidogo sana.Ndiyo… mayai ni chanzo kizuri kabisa cha protini, huku yai moja likiwa na gramu 6 za protini.
 
Kula kiasi cha kutosha cha protini kunaweza kuwa msaada katika kupunguza uzito, kuongeza uwingi wa mishipa, kupunguza shinikizo la juu la damu na kuimarisha afya ya mifupa, kwa kuyataja machache kati ya mengi ya faida ya ulaji wa kutosha wa protini.
 
Tafiti nyingi zaidi na zaidi zimeendelea kutoa hitimisho hili moja linalofanana.

Ingawa… baadhi ya tafiti zimeweza kuonyesha kuwa watu wenye kisukari hasa wenye kisukari cha aina ya pili wanaokula zaidi mayai wanakuwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…