Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo
 
B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu.
 
B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.
 
B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.
 
Vyakula vya vitamini B
Tunaweza kupata vitamini B kwenye vyakula vifuatavyo:-
1.Nyama
2.Nafaka kama mchele, mtama, mahindi n.k
3.Mimea jamii ya maharagwe kama kunde
4.Viazi
5.Ndizi
6.Pilipili
7.Mayai
8.Mimea jamii ya karanga na alizeti
9.Mboga za majani zenye kijani iliyowiviana na kutia weusi kama spinachi
10.Matunda kama palachichi na ndizi
 
Dalili za upungufu wa vitamini B
1.Kupata ugonjwa wa Anaemia huu ni upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini
2.Matatizo kwenye ngozi
3.Kupata vidonda kwenye mdomo, ma kupasuka kwa mdomo
4.Misongo ya mawazo ama kuchanganyikiwa
5.Kuharisha
6.Kupotesa kumbukumbu kwa urahisi
7.Misuli kupoteza ujazo
8.Kubadilika badilika kwa mood (fikra na hisia) yaani mara umekasirika mara umefurahi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…