Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye pingili za mgongo na tumboni pia hakutakiwi kufanyiwa tiba hiyo kutokana na muundo wake,” anasema.

Dk Lamila anasema ‘hard massage’ hufanywa kwa wanamichezo na ikitokea mtu wa kawaida akafanyiwa inaweza kuumiza misuli yake na matokeo yake kupata madhara yanayoweza kumletea ugonjwa.
 
Hilo linaungwa mkono na Mfizotherapia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Abdalla Makalla anayeeleza kuwa yapo madhara makubwa kiafya endapo ‘massage’ itafanywa bila kujua historia ya anayefanyiwa.

Hata hivyo, Dk Makalla anasema zipo aina mbili za ‘massage’ moja ikiwa ni ile ya tiba na nyingine ya kuondoa uchovu.
 
Pia, anaeleza kuwa mtu mwenye tatizo la damu yake kuganda na kutengeneza donge la damu kitaalamu inafahamika kama DVT Deep vein thrombosis, naye anatakiwa kujiweka kando na huduma hii.

Ikitokea mtu mwenye tatizo hilo akafanyiwa ‘massage’ kuna uwezekano wa bonge hilo kusafirishwa na kwenda katika sehemu nyingine ambazo hazitakiwi kuzibwa kama kwenye moyo au mapafu.
 
Anasema, “Ikitokea mtu shinikizo lake la damu limepanda asije kukimbilia kufanya ‘massage’ akifikiri ndiyo atapata unafuu hiyo itamletea athari zaidi.

“Hii ina maana kwamba presha ikiwa juu halafu ukaifanya damu iende kwa kasi ni kuongeza tatizo juu ya tatizo,” anasema Dk Makalla.
 
Pia, anaeleza kuwa mtu mwenye tatizo la damu yake kuganda na kutengeneza donge la damu kitaalamu inafahamika kama DVT Deep vein thrombosis, naye anatakiwa kujiweka kando na huduma hii.

Ikitokea mtu mwenye tatizo hilo akafanyiwa ‘massage’ kuna uwezekano wa bonge hilo kusafirishwa na kwenda katika sehemu nyingine ambazo hazitakiwi kuzibwa kama kwenye moyo au mapafu.
 
Pia kama mtu mwenye saratani ya aina yoyote atakiwi kujihusisha na hilo kwa kuwa ataifanya isambae hata katika maeneo ambayo ilikuwa haijafika na hilo litamfanya siku zake za kuishi kupungua kutokana ugonjwa kusambaa mwilini kwa kasi,” anasema Dk Makalla
 
Kuna watu mitaani huko wanadai kwamba wanawafanyia ‘massage’ kunyoosha viungo hasa kwa watoto wenye mtindio au wagonjwa wa kiharusi, niwaleze wazi kuwa kazi hiyo inafanywa na wataalamu tu, hao wa mitaani wanaongeza mkakamao,” anasema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…