Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umewahi kusikia kuhusu Mwezi wa Samawati au Buluu ambao kwa Kiingereza huitwa Blue moon? Matumizi ya msemo huu yanaaminika kuanzia mwaka 1883 kufuatia kulipuka kwa mlima wa volkano wa Krakatoa nchini Indonesia. Vumbi kubwa lilijaa angani hivi kwamba wakati uliuangalia Mwezi, ulionekana kama ulikuwa na rangi ya samawati.
 
Imani za kale za Kichina zilisema kuwa kupatwa kwa jua kulisababishwa na joka kulimeza jua.

Kuzuia hilo watu walipiga kelele sana wakati wa kupatwa kwa jua kumfanya joka aogope na atoroke.
 
Pia waliamini kuwa chura mkubwa aliishi kwenye Mwezi akiketi juu ya shimo kubwa. Mashimo makubwa kwenye Mwezi hayakusababishwa na wanyama wowote bali yalisababishwa na mawe makubwa ya anga za juu kuugonga mwezi takriban miaka bilioni 4.1 iliyopita.
 
6. Mwezi unapunguza kasi ya dunia.

Wakati mwezi unakaribiana sana na dunia kile kinachaoitwa Perigee hutokea. Hii inamaanisha kuwa nguvu za kuzunguka kwa dunia hutwaliwa na Mwezi kidogo kidogo hali ambayo husababisha dunia kupunguza kasi yake kwa karibu milisekunde 1.5 kwa kila karne moja
 
7. Mwangaza wa mwezi

Jua lina mwangaza wenye nguvu mara 14 zaidi ya ule wa Mwezi unapokuwa mpevu. Ili Mwezi mpevu upate kuwa na mwangaza sawa na wa jua unahitaji kuwa na Miezi 398.110. Wakati wa kupatwa kwa Mwezi wakati mwezi unaingia kwenye kivuli cha dunia viwango vya joto mwezini vinaweza kushuka hadi karibu nyuzi joto 500F (260 celsius) katika kipindi cha chini ya dakika 90
 
8. Leonardo da Vinci aligundua kuwa mwezi haukuwa na umbo la hilali

[https://ichef]

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Wakati Mwezi unaonekana kuwa umbo la hilali, kile tunachokiona ni mwanga wa jua ukimulika sehemu ya Mwezi. Eneo jingine la mwezi halionekani vizuri, kulinngana na hali ya hewa. Leonardo da Vinci ndiye mtu wa kwanza anayejulikana kugundua kuwa mwezi haukuwa unapungua au kuongezeka. Ni kuwa sehemu yake nyingine ilikuwa imefichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…