AC Milan ina hamu ya kuwasajili wachezaji watatu wa Chelsea winga wa Morocco Hakim Ziyech, 28, na wachezaji wawili wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, na Tiemoue Bakayoko, 26, wote wakinyatiwa. Bakayoko alihudumu msimu wa 2018-19 kwa mkopo akiwachezea mabingwa hao wa Itali. (Di Marzio via Sempre Milan)
Klabu za Leeds United, West Ham na Southampton zote zinamuwania beki wa Barcelona Junior Firpo, 24, huku mchezaji huyo wa Uhispania akitaka kuondoka katika uwanja wa Nou Camp mwisho wa msimu ujao. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Na klabu ya Barcelona itamlenga Marcos Alonso wa Chelsea ,30, iwapo Firpo angeondoka , Ijapokuwa Inter Milan pia inachunguza hali ya beki huyo wa Uhispania katika uwanja wa Stamford Bridge. (Mundo Deportivo - in Spanish
Ifikiapo mwaka 2024, iwapo mambo yatafanyika kulingana na mipango iliowekwa na Marekani, Utawala wa rais Joe Biden utapokea ndege mpya aina ya Airforce One .
Ndege hiyo ilioundwa kwa lengo la kivita ina uwezo wa kuhimili mshindo wa mlipuko wa kinyuklia. Iwapo mlipuko wa bomu hilo ungetokea rais wa Marekani angeepuka .