Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baadhi ya watu hufikiri kuwa ili uweze kuweka akiba ni lazima uwe na pesa nyingi, kuweka akiba ni kanuni mojawapo ya matumizi mazuri ya pesa.
 
Ikiwa umekuwa ukipuuza suala la kuweka akiba na kuliona kuwa halina maana Fahamu faida kuweka akiba ya fedha.
 
Utulivu wa akiliUnapokuwa huna akiba yoyote huwezi kuwa na utulivu wa akili. Kila wakati unahofu na wasiwasi juu ya maisha yako, unajiuliza likitokea tatizo itakuaje? Au hitaji fulani linalokuja hivi karibuni litakuwaje?
 
Hukuwezesha kuwahi fursaNi mara ngapi umekuwa ukisema au ukisikia kauli kama vile “Ningekuwa na pesa ningenunua hiki kitu”, “Ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye hii huduma”, “Ningekuwa na pesa ningejiunga na huu mradi”, n.k.
 
Unapokuwa na akiba ya fedha ni rahisi kuwahi fursa mpya au bidhaa zenye manufaa mara zinapopatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…