Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na pesa, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani.
Serikali ya Kenya sasa inatarajia kulegeza masharti ya afya yaliyowekwa kufuatia mlipuko wa janga la UVIKO-19 miaka miwili iliyopita ikiwemo uvaaji wa Barakoa.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema hayo kwenye mahojiano na kituo cha Citizen TV, Machi 9, kwamba ataondoa sheria ya ulazima ya kuvaa barakoa kufuatia kupungua kwa makali ya maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.
Kagwe ameeleza kuwa licha ya kupuuzwa kwa wazi kwa sheria hizo, rekodi ziko chini kuashiria kuwa raia wana kinga thabiti na Wizara yake bado inaendelea na utafiti wake na inatarajiwa kutoa tangazo kuhusu kusahisishwa kwa sheria hizo siku chache zijazo.
Mara ya kwanza nilipogundua hawa watu siku hizi hawajavaa barakoa basi unajiuliza nini kinafuata?, tuangalie tuone. Labda tunaendelea kuwa na kinga yenye nguvu polepole na tunapoendeleza kinga hiyo, hauwi mkali kwao. Hautumii polisi kuwapiga kwa sababu hawajavaa maski,” alisema Kagwe
Pia aliongezea akisema kuwa, “Ikiwa hawaugui, basi labda huo ndio mwelekeo tunaopaswa kwenda. Huu ni uamuzi ambao tutafanya katika siku chache zijazo.”
Waziri huyo pia alieleza kuwa baadhi ya utafiti unaofanywa ni kuhakikisha kwamba kiwango chanya cha maambukizi kiko chini kwa muda fulani na kwamba hospitali zina vifaa vya kutosha iwapo kutakuwa mlipuko wa homa hiyo tena.
Haya yanajiri huku Kenya ikirekodi kiwango chanya cha asilimia 0.3 mnamo Jumatano, Machi 9, baada ya watu 14 kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona kutoka kwa sampuli 5,585 zilizopimwa.
Rekodi za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa ni watu 27 tu ndio wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku 204 bado wako chini ya uangalizi wa nyumbani.
Hospitali hiyo ilitangaza Jumatano, Machi 9, kuwa David Bennett, 57, alikata roho mnamo Jumanne, Machi 8, katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Maryland
Bennett, ambaye alikuwa na tatizo la ugonjwa wa moyo, alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza moyo huo mnamo Januari 7 na upandikizaji huo unadaiwa ndio ulikuwa njia pekee ya matumaini ya kuokoa maisha ya Bennett ikiwa wakati huo madaktari wa Chuo Kikuu cha Maryland walipewa idhini maalum na wasimamizi wa matibabu kuendelea na upasuaji huo, kwa misingi kwamba Bennet angelipoteza maisha yake.
Mwanaume huyo alikuwa akionekana hakuwa na uwezo wa kupandikizwa moyo wa binadamu, uamuazi ambao huchukuliwa na madaktari wakati afya ya mgonjwa inapozorota zaidi.
Nguruwe aliyetumiwa katika upandikizaji huo alifanyiwa mabadiliko ya vinasaba ili kuondoa jeni kadhaa ambazo zingefanya kiungo hicho kikataliwe na mwili wa Bennet.
Hata hivyo Madaktari waliofanya upandikizaji huo, walisema endapo yangekuwa ni mafanikio yangehitimisha miaka kadhaa ya utafiti na kubadili maisha kote duniani na ni hatua moja ya kukaribia kutatua mzozo wa ukosefu wa kiungo cha mwili.