Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baadhi ya makabila wamekuwa wakiwaua kwa kutumia mikuki lakini wengine wameenda mbali zaidi na kutumia sumu kwenye mizoga hivyo kupelekea kuuwawa kwa aina/ spishi nyingi tofauti zinazotumia nyama na mizoga kama Tumbusi na Fisi.
 
Wanyama hawa wanapitia wakati mgumu pale wanapo winda mifugo au wanyama wengine wa pori ambao walikuwa na maingiliano nao hivyo kuambukizwa magonjwa kama Kimeta na kichaa cha mbwa ambayo yanaua kwa kasi kubwa na kusambaa haraka.
 
Sababu zitokanazo na miingiliano yao katika utafutaji wa mahitaji yao,

Wanyama wanokula nyama jamii ya samba hususani dume wamekuwa na tabia ya kuuwa watoto wa samba jike ambao sio wa kwake.
 
mfano jinsi gani Simba dume akivamia familia ya dume mwingine Kuuana kama njia ya kupunguza ushindani, pasipo kujali huyu ni Simba, Chui, Fisi, Duma au Mbwa mwitu.
 
Kupigana na kuumizana kipindi wanatafuta majike, hii inaonekana zaidi kwa Simba ambapo mara nyingi madume wamekuwa wakipigana na kuumizana na wakati mwingine kuuana wakati wanatafuta majike ili kuzaliana.
 
Simba jike ndo wawindaji hivyo baada ya kuwinda hula pamoja familia na nzima kitu ambacho ni tofauti kwa Mbwa mwitu hawa maisha yao kidogo ni magumu baada ya kuwinda hurudi katika familia zao na hutapika chakula ili kuwalisha watoto wao. Hivyo wawindaji wanakuwa na wakati mgumu sanaaa na mara nyingi huishia kufa kwa njaa.
 
Sababu zitokanazo na mawindo yao,

Kuhama kwa mawindo yao, wanyama walao nyama wamekuwa kwenye wakati mgumu pale mawindo yao yanapohama kwa lengo la kutafuta sehemu nzuri kwa ajiri ya kuzaliana na kwenye malisho mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…