Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Juventus wanalenga kuwanunua wachezaji wawili wa kimataifa wa Italia wa Chelsea - kiungo Jorginho, 30, na beki wa kushoto Emerson Palmieri, 27, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Lyon. (Tuttosport - in Italian)
 
Barcelona pia wanaifuatilia Chelsea na wanavutiwa na wachezaji wao wawili wa kimataifa wa Uhispania - mlinzi wa kushoto Marcos Alonso, 31, na mlinzi wa kulia Cesar Azpilicueta, 32, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu. (Mundo Deportivo)
 
Ombi la Saudi Media la kutaka kuinunua Chelsea ni pamoja na mipango ya kuunda upya Stamford Bridge na kuwaongezea kandarasi wachezaji kama vile Azpilicueta na mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger, 29, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kuisha msimu huu wa joto. (Goal)
 
Mkufunzi binafsi wa Paul Pogba anasema kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 28, ataondoka Manchester United mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Calciomercato)
 
Newcastle wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Sean Longstaff, kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu. Mchezaji huyo 24, mkataba wake unamalizika msimu wa joto (Times)
 
Manchester United wanaweza kuchukua hatua ya kumrejesha Sam Johnstone kutoka West Brom msimu wa joto, ingawa Tottenham na Southampton pia wana nia ya kumsajili mlinda mlango huyo wa England mwenye umri wa miaka 28, ambaye anatazamiwa kuwa mchezaji huru. (Sun)
 
Chelsea imeiomba serikali ya Uingereza kuondoa marufuku ya kuwaongezea mikataba wachezaji huku kukiwa na hofu kuwa huenda ikawaacha na mzozo mkubwa wa ulinzi msimu ujao. (Telegraph )
 
Manchester United wamejulishwa kuhusu uwezekano wa kocha wa Chelsea Thomas Tuchel kupatikana mwishoni mwa msimu huu. (Mail)
 
Real Madrid wanataka kumbakisha kiungo wa kati wa Croatia Luka Modric, ambaye anatazamiwa kuwa mchezaji huru kwa angalau msimu mwingine lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 bado hajasaini mkataba mpya. (Marca- in Spanish)
 
Juan Mata anaweza kupewa nafasi ya ukocha katika klabu ya Manchester United - ikiwa kiungo huyo wa kati wa Uhispania, 33, atastaafu mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto. (Sun)
 
Mshambuliaji Luis Suarez ataondoka Atletico Madrid msimu huu wa joto mkataba wake utakapomalizika, huku mabingwa wa Italia Inter Milan pamoja na Ajax, Sevilla na klabu kadhaa ambazo hazijatajwa nchini Brazil zikiwania kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 35. (Marca - in Spanish)
 
Aston Villa wanamfuatilia kiungo wa kati wa Paris St-Germain Georginio Wijnaldum na wameambiwa kiungo huo wa kimataifa wa Uholanzi wa miaka 31-atagharimu pauni milioni 21. (Sport, via Sun)
 
Newcastle wako tayari kuweka mezani ofa ya £50m kumnunua winga wa Bayer Leverkusen Moussa Diaby, 22, ambayo iko chini ya hesabu ya klabu hiyo ya Ujerumani kwa mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa ya takriban £75m. (Mail)
 
Paris St-Germain wanataka kumsajili tena mshambuliaji wa Everton Moise Kean, ambaye yuko Juventus kwa mkopo hadi msimu wa joto wa mwaka 2023. (Calciomercato - in Italian)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…