Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Barcelona inataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu, mkataba wake utakapomalizika. (Sport)
 
Paul Torres wa Villarreal amerudi kwenye rada za Manchester United ambao msimu uliopita walizingumza na mlinzi huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 25, kabla ya kuamua kumsajili Raphael Varane. (90min)
 
Manchester City wana matumaini ya kuwashinda Real Madrid katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21 msimu huu. (ESPN)
 
Newcastle United inataka kumsajili kiungo wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, 29 ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Aston Villa.(Sport)
 
Arsenal imekua ikiwafuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 23, na mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 24. (CBS Sports)
 
Aston Villa wanajiandaa kuvunja tena rekodi yao ya usajili msimu huu huenda wakatumia zaidi ya Β£150m kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya. (Football Insider)
 
Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel "ana uhakika" klabu hiyo itaweza kushughulikia suala la mkataba mpya wa mlinzi wa kijerumani Antonio Rudiger, 29. (Goal)
 
Leeds wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa Marekani Brenden Aaronson, 21, mazungumza yakiendelea kwa ajili ya uhamisho wake mwishoni msimu akitokea RB Salzburg. (Football Insider)
 
Mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa wa kusalia West Ham kwa kiungo wa Czech Tomas Soucek, 27, yamesimama mpaka mwishoni mwa msimu, licha ya kusakwa na vilabu vikubwa Ulaya. (90min)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…