Barcelona wamepanga kukutana na wakala wa Ousmane Dembele kuhusu mkataba mpya wa winga huyo wa Ufaransa, 24, ambaye alitarajiwa kuwa mchezaji huru msimu wa joto. (Marca)
Manchester United inaweza tena kuzingatia uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 29. (Corriere dello Sport, via Express)
Wakati mkataba wa sasa wa Juan Mata wa Manchester United ukimalizika mwezi Juni kiungo huyo wa zamani wa Uhispania, 33, hana mpango wa kustaafu au kujiunga na timu ya ukufunzi wa United. (Fabrizio Romano, on Twitter)