Ni wazi kuwa tunatenda mema kwa sababu vitabu vya dini vinatushauri kutenda mema na kutusisitiza kuwa ukitenda mabaya kuna adhabu yake baada ya mwisho wa maisha ya hapa duniani.
Lakini pia kwa mtazamo mwingine tunatenda mema kwa sababu kuna manufaa kwetu, watu wanaotuzunguka, viumbe vinavyotuzunguka, ndugu, na mazingira katika Maisha haya haya ya sasa hapa hapa duniani.
Fikiria kama ingekuwa ni ruhusa kuua, kuiba au kufanya matendo ya kiovu bila kuwa na kosa, watu wengine ambao wangetendewa mabaya hayo wangekuwa wanapata taabu.