Mkuu wa Borussia Dortmund Sebastian Kehl anasema Manchester City hawajafikia mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21. (Mail)
Kahn pia amethibitisha kuwa klabu hiyo iko kwenye mazungumzo ya mkataba na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Poland Robert Lewandowski, 33. (Sport, via 90 Min)
West Ham wako tayari kutoa dau la kumnunua mlinzi wa Manchester United Muingereza Di'Shon Bernard,21, ambaye kwa sasa anachezea Hull kwa mkopo. (Mirror)
Tottenham wanamfuatilia mchezaji wao wa zamani na kiungo wakati wa sasa wa Brentford Christian Eriksen, 30. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmarkanapania kurejea Spurs. (Football Insider)
Hata hivyo Gunners huenda wakamkosa kiungo wa kati wa RB Leipzig Christopher Nkunku baada ya Inter Milan kuongeza juhudi za kumpata Mfaransa huyo wa miaka 24. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Newcastle wanajiandaa kufufua tena mpango wao wa kumsaka beki wa Torino Gleison Bremer. Kiungo huyo wa Brazil wa miaka 25- pia nanyatiwa na Arsenal na Tottenham. (Tuttomercato - in Italian)