Ukianzia na vyakula vyenye asili ya wanyama (Mfano nyama na samaki), vyenye asili ya mimea Mfano matembele, bamia, mchicha, bilinganya na vinavyo fa nana na hivyo na vyakula vitokanavyo na mbegu za mimea mbalimbali mfano karanga, korosho, ufuta n.k.
Faida za supu ni nyingi, kwa ufupi ni kama ifuatavyo: Supu husaidia kuamsha hamu ya kula kwa yule aliyekuwa hana na humuongezea hamu ya kula kwa yule aliyenayo. Na hii hasa hupatikana iwapo supu itakuwa na viungo mbalimbali vyenye harufu na ladha tofauti.