Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Put yourself in God’s hands tonight and pray that He will lead you in the right direction. Then simply let go and trust Him, believing that you will sense God's direction and that He will bring you the peace you need. David C. Cook,
 
Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.
 
Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.
 
Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi huwa na kirutubisho kinachojulikana kama ‘tryptophan,’ ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha
 
Mbali na kusaidia wakina mama katika matatizo ya hedhi pia ndizi huweza kuwasaidia watu ambao husumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu (anemia), hii ni kwasababu ndizi imekuwa ni chanzo kizuri cha madini ya aina ya chuma (iron), hivyo inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya tatizo la upungufu wa damu kwasababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.
 
Ama hakika tunda hili ni la kipekee kwani pia huweza kusaidia kukabiliana na tatizo la shinikizo la damu kwani lina kiwango kikubwa cha madini ya ‘potassium’ na wakati huo huo pia tunda hili lina kiasi kidogo cha chumvi ‘sodium
 
na hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu na katika kuonesha uwezo wa tunda hili juu ya kusaidia kukabilina na shinikizo la damu ni pale ambapo miaka ya hivi karibuni Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani iliamua kuwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.
 
Sambamba na faida hizo za tunda hili pia inaelezwa huweza kusaidia kupunguza Kasumba yaani 'hangovers' ndizi ni moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangovers) , hivyo unaweza kunywa ‘milk shake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…