Kocha wa Barcelona Xavi anataka kusalia na kiungo wa kati wa Mholanzi Frenkie de Jong, 24, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United ambao utamkutanisha tena na mkufunzi wake wa zamani Erik ten Hag. (Manchester Evening News)
West Ham itajaribu kumsaini mchezaji wa safu ya kati na nyuma Michael Keane, 29, kutoka Everton ikiwa Toffees wataondolewa katika Ligi ya Primia msimu huu. (Star Sunday)
Napoli wanataka angalau euro 80m (£67m) ikiwa wataamua kumuuza mshambuliaji wa umri wa miaka 23 Victor Osimhen, ambaye ni miongoni mwa walengwa wa Arsenal msimu huu wa joto. (CBS Sports)
Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Rodrigo de Paul, 27, anataka kurejea Italia na anafuatiliwa na Inter Milan. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Arsenal inamsaka mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, 25, kumpeleka Emirates, huku tayari mkurugenzi wa ufundi wa 'the Gunners' Edu ameshafanya mazungumzo na wawakikishi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Athletic, subscription required)
Mo Salah anataka kusalia Liverpool lakini hatma yake ya muda mrefu bado ni tata na wakati mkataba ukiwa bado kufikiwa mshambuliaji huyo wa Misri, 29 anasema pesa sio jambo pekee kuhusu hatma yake. (Four Four Two)
Paris St-Germain imempa mshambuliaji mfaransa Kylian Mbappe, 23, mkataba wenye thamani ya £42m kwa mwaka, utakaomfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo.
Mama yake na Mbappe na mwakilishi wake Fayza Lamari yuko Qatar kufanya mazungumzo na wamiliki wa holding PSG (Le Parisien - in French, subscription required)
Kocha wa Tottenham Antonio Conte anataka kuinoa PSG msimu ujao akiwa na uhakika wa kurithi mikoba ya kocha wa zamani wa Spurs Mauricio Pochettino pale Parc des Princes. (Le Parisien - in French, subscription required)