Baada ya miaka ya majadiliano, Singapore ilitangaza mwezi uliopita kwamba ingeondoa marufuku kwa wanawake wasio na waume ambao wanataka kugandisha mayai yao kwa sababu zisizo za kiafya.
Lakini wakati wengi wamefurahishwa na kukaribisha hatua hizo, wengine wanasema bado kuna mengi yanayohitajika katika utaratibu huo na yanaonyesha Singapore bado ina safari ndefu kabla ya sera hiyo kuzingatiwa kuwa inajumuisha kila mmoja.
Mnamo mwaka 2020, Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Familia ya nchi hiyo, ilisema walipaswa kuzingatia ''maswala ya kimaadili na kijamii juu ya kuhalalisha kugandisha yai'', miongoni mwa mambo mengine.
Walakini, mwezi uliopita, katika hatua ya msingi, serikali ilitangaza kwamba kuanzia 2023, wanawake wasio na waume wenye umri kati ya 21-35 wataruhusiwa kugandisha mayai yao.
Hii haijumuishi mara moja wanawake wasio na waume ambao wanaweza kutaka kulea watoto nje ya ndoa na pia wapenzi wa jinsia moja ambao hawawezi kuolewa chini ya sheria za Singapore.