Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Virutubisho vya moja kwa moja vyenye madhara :Asilimia 10 hadi 25 ya watu hupata madhara kutokana na aina fulani za vyakula katika nchi zilizoendelea.
 
Hukuzuia kuharibu chakula:
Lebo za chakula zikisomwa kwa usahihi zinakusaidia usitupe chakula unachohofia.
Siku chakula kilipotengenezwa na siku ya mwisho ya matumizi hukusaidia kufahamu bidhaa hiyo itakuwa salama kuliwa kwa kipindi gani.
 
Inakusaidia kuepuka magonjwa kutokana na kula chakula kilichopitwa na wakati. Hata hivyo, kuchanganya maneno “bora kabla” na “tumia hadi” tarehe zinaweza kusababisha uharibifu wa chakula zaidi.
 
Barani Ulaya, karibu 10% ya chakula kinachoharibiwa kinahusishwa na tarehe. Kufelimisha watumiaji na wanunuzi wote unaweza kusaidia kuzuia uharibifu wa chakula na kuhakikisha tarehe sahisi kwa sababu yakuhakikisha chakula kipo salama kwa mlaji.
 
6. Kuunga mkono chakula cha kienyeji au kinachozalishwa na wenyeji:
Lebo fulani ambazo huonesha asili ya chakula, kwa mfano kahawa ya Colombia yani Columbian Coffee (Colombia), Jibini ya Manchego (Spain), chai ya Darjeeling (India) au kahawa ya Kona (USA), vinaweza kuvutia wateja na kuongeza thamani kwa bidhaa kwa wazalishaji.
 
Walaji hupenda kutambua bidhaa za kienyeji katika sehemu fulani na sifa zake kwa mfano ladha na ubora kuhusiana na sehemu fulani bidhaa zinapozalishwa. Katika utafiti uliofanywa na EBRD kwa ushirikiano na FAO, bidhaa za kiasili 9 zilioneshwa lebo hizo zilisaidia bei ya bidhaa hizo kuongezeka kwa silimia 20 hadi 50, leo wateja wake wameongezeka wakihusishwa na makaazi yao ya kijiografia, ubora na utamaduni.
 
Lakini ni muhimu kufahamu kwamba habari ni nguvu na pia nguvu hizi zinaweza kukusaidia kulinda afya yako.
 
Huenda usipende kuitwa “mwenye msimamo mkali kuhusu afya” au “mtu anayependa sana chakula cha viwandani”, lakini unataka nyanya zako ziitwe nyanya na karanga zako kuitwa karanga!
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…