Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dalili za upungufu wa wanga

Kudumaa kiakili na mwili

Kukonda na kupungua uzito

Ngozi kusinyaa na kukunjamana, mtoto huonekana kuwa amezeeka

kuhara kunaweza kukawepo.
 
Madhara ya kuzidi kwa wanga

Kuongezeka uzito


Wanga nayozidi mwilini hubadilishwa kuwa mafuta na kuhifadhiwa sehemu mbalimbali za mwili. Hii huweza kuchangia uzito kupita kiasi.
 
Madhara ya kuzidi kwa wanga

Kuongezeka uzito


Wanga nayozidi mwilini hubadilishwa kuwa mafuta na kuhifadhiwa sehemu mbalimbali za mwili. Hii huweza kuchangia uzito kupita kiasi.
 
Kuongeza hatari ya ugonjwa wa sukari katika umri mkubwa


Vyakula vya wanga kwa wingi huchochea kongosho kuzalisha homoni ya insulin kwa wingi ili kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu.
 
Baada ya muda mrefu kongosho huweza kuchoka na kushindwa kuzalisha homoni hii na hivyo kupelekea kuongezeka kwiango cha sukari na mwisho kupata ugonjwa wa sukari.
 
Kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo na shinikizo la juu la damu


Wanga iliyozidi mwilini na kubadilishwa kuwa mafuta huweza kujikusanya kwenye mishipa ya damu na kupelekea magonjwa ya moyo.
 
Kuoza meno


Kula wanga kwa wingi kunaongezaatari ya meno kuoza kwani bakteria waliopo mdomoni humeng'enya mabaki ya wanga na kutengeneza tindikali ambayo huozesha meno kwa kusabisha mashimo madogomadogo kwenye meno.Kuepuka hili ni muhimu kuswaki angalau mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…