Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mboga za majani hubeba kwa wingi vitamin, madini na nyuzinyuzi zinazosaidia mfumo wa chakula kumeng’enya chakula. Faida za mboga za majani hutegemea aina ya mboga ya majani.
 
Aina mbalimbali za mboga za majani na faida zake

Spinach


Mboga hii ya majani huwa na wingi wa madini chuma, kalisiamu, magnesium na Folate Pamoja na antioksidanti, Vitamin K, A na Vitamin C, madini na vitamin zilizo kwenye mboga hii humpa mtu uwezo wa kuona vizuri, kuimarisha mifupa na kusaidia damu kuganda mapema unapoumia
 
Kale


Ni mboga ya majani jamii ya kabeji, mboga hii hutoa nishati,vitamin A na C pamoja na K , husaidia kupunguza mafuta kwa wingi na uzito ikitumiwa kama juisi pia hupunguza shinikizo la juu la damu.
 
Kale


Ni mboga ya majani jamii ya kabeji, mboga hii hutoa nishati,vitamin A na C pamoja na K , husaidia kupunguza mafuta kwa wingi na uzito ikitumiwa kama juisi pia hupunguza shinikizo la juu la damu.
 
Broccoli


Ni mboga ya majani jamii ya mboga kabeji, Mboga hii huwa na nishati kwa wingi, Vitamin C na K, kula kwa wingi mboga hii huweza kupelekea kupunguza hatari ya magonjwa ya saratani ,Mboga hii hupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…