Au mkaseme: Lau tungeliteremshiwa Kitabu basi bila shaka tungelikuwa tumehidika zaidi kuliko wao. Kwa yakini imekwishakufikieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu na mwongozo na rahmah. Hivyo basi nani ni dhalimu zaidi kuliko yule aliyekadhibisha Aayaat za Allaah na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Aayaat Zetu adhabu ovu kwa sababu ya kujitenga kwao.
Je, wanangojea nini isipokuwa Malaika wawafikie (kuwatoa roho), au Awafikie Rabb wako (kuwahukumu)[ au ziwajie baadhi ya Aayaat (Ishara, Alama za Qiyaamah) za Rabb wako? Siku zitakapokuja baadhi ya Aayaat za Rabb wako haitoifaa nafsi imaan yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika imaan yake kheri yoyote. Sema: Ngojeeni hakika nasi tunangojea.
Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi, wewe huhusiki nao kwa lolote. Hakika kesi yao iko kwa Allaah, kisha Atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi Ameniongoza Rabb wangu kuelekea njia iliyonyooka, Dini iliyosimama thabiti, mila ya Ibraahiym aliyejitenga na itikadi potofu na kuelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.