Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati mwingine tunapitia njia tofauti ili kutimiza ndoto na malengo tuliyojiwekea katika maisha yetu ya kila siku. Sio mpaka wote tuonekane kwa pamoja. Tambua, njia yako sio njia ya mwenzio pia. Kila mtu atang'ara kwa wakati wake. Amini tu.
 
Haijalishi mambo ni magumu kiasi gani upande wako. Siku zote tunza amani yako ya ndani. Hiyo ndio nguvu yako kubwa. Bila hiyo wewe si chochote wala lolote. Kumbuka, hakuna kinachodumu milele. Kila kitu kitapita katika maisha haya ya mpito. Amini. Tumaini. Usikate tamaa.
 
Watu wanapitia mengi sana ambayo hatuyaoni wala hawatuonyeshi usoni mwetu. Ukiwakuta watu wanafurahi ama kushangilia mafanikio yao hata kama ni madogo, ama ungana nao kushangilia, au wapishe washangilie. Kama wewe si sehemu ya maumivu yao, usilazimishe kuwa sehemu ya furaha yao.
 
Kukosa msaada. Kupoteza matumaini. Kukosa nguvu. Sote tunapitia hivyo. Lakini kukata tamaa sio nia yetu kuu. Matumaini ndio yanatuweka hai mpaka sasa. Haijalishi nini kinaendelea upande wako. Ila kuamini, kujua kwamba Mungu yupo nasi kila wakati ni faraja ya kuendeleza mapambano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…