myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 166,767
- 705,461
ππkatika Maisha siyo kila siku watu wanakuwa na fedha, muda mwingine wanakuwa hawana pesa, tusiwafikilie vibaya!
Maisha ni hatua, kila mtu ana zake, usitamani na kuchukia hatua za mwenzako, pambana na hatua zako, kuna hatua ndefu na fupi, hatua zako ukizipambania zitakuwa ndefu, unaemuona leo Kapiga hatua ndefu alizipambania, usimchukie jifunze na kumdadisi aliwezaje kuwa na hatua ndefu
Katika Maisha Kila Mtu Ana Juhudi Zake Za Kupambana , Kuna Waliofanikiwa Na Ambao Wako Katika Mnyororo Wa Mafanikio, tabia ya Baadhi ya Watu Kuhisi Kwamba Waliofanikiwa wote Wamebebwa Inafanya Wao Wasifanikiwe Kwa Kutopambana na kuamini kwamba hawawezi fanikiwa pasipo kubebwa
βοΈβοΈ
Maisha ni kama safari,na ili ufanikiwe lazima uweke Juhudi,
β οΈβ οΈ
Kila mwaka unatarehe na mwezi wa kifo chako unafanikiwa kupita, Ila kuna mwaka hauta pita, Mimi na wewe hatujui ni lini Tumuombe Mungu Atupe Mwisho Mwema
Tuliza moyo wako, Kubali mapungufu yako, Rahisisha mahitaji yako, Ridhika na ulichonacho, Ongeza kipato chako, Chunga tamaa mbaya.
ππWakati barabara inakuwa ngumu, kumbuka kuwa hatua za mtu mwema huongozwa na barabara. Songa mbele kila hatua sala
Tuliza moyo wako, Kubali mapungufu yako, Rahisisha mahitaji yako, Ridhika na ulichonacho, Ongeza kipato chako, Chunga tamaa mbaya.
Hatima ya maisha yako mwenyewe inaanzia kwenye mindset yako na jukumu la kujenga au kubomoa linaanzia kwako