Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jamii inataka uwe dhaifu na depressed.
Chagua vita zako vyema.
Sio kila kitu kwenye jamii ni cha kufata.
 
Pambana kuhakikisha jamii inakuzingatia.
Kuwa na misimamo, misingi na falsafa zako.
 
Kwenye kutafuta pesa, ONDOA AIBU. Usipokuwa makini, utalala njaa na uwezo, kipaji na ujuzi wako. As long as una kitu cha thamani, simamisha dunia isikie kuwa kuna thamani unayo. (Kumbuka usiwahi tweza utu wako - Be vigilant).
 
Chagua marafiki vizuri. Ni bora kutokuwa na marafiki kama wote ulio nao hawakujengi zaidi ya kula energy yako. Kuwa na marafiki wanaoongeza thamani maishani mwako.
 
Kuwa imara na control hisia zako. Kiumbe unaeweza kucheza na hisia zake, ni dhaifu sana.
Unatakiwa kuwa juu ya hisia zako kwenye kila hali.
 
Nidhamu ya maisha ndio kila kitu. Usiwahi kuwa mtu wa kujisikia kufanya vitu. Unahitaji kupigania maisha yako na nidhamu ya kama upo kwenye state of urgency.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…