Mh Edward Lowassa amesema licha ya changamoto nyingi anazopata akiwa ndani ya upinzani, atagombea tena urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na anaamini atashinda. Lowassa aliyejitokeza kugombea urais kupitia CCM mwaka 2015 na jina lake kukatwa kisha kuhamia Chadema alikogombea nafasi hiyo akiwakilisha vyama vilivyoungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kushindwa na Rais John Magufuli, bado anatajwa kuwa mgombea mwenye nguvu katika kambi ya upinzani. Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rais Magufuli alishinda kwa kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46, huku Lowassa wa Chadema akijipatia kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97 ya kura zote. Akizungumza jana katika mahojiano maalumu na waandishi wa Nation Media Group (NMG) jijini Nairobi, Lowassa alisema, “Kwa mapenzi ya Mungu nitajaribu tena mwaka 2020 na nitapita kwa mikono safi.” Kama ambavyo amekuwa akisema tangu aliposhindwa katika uchaguzi huo wa 2015, pia jana Lowassa alisema licha ya kuendeshwa katika mfumo usioaminika, hakutaka kuwashawishi wafuasi wake wamwage damu kwa kudai ushindi. “Wafuasi wangu walitaka tuingie mitaani kudai ushindi, lakini kulikuwa na bunduki nyingi mikononi mwa wanajeshi. Niliogopeshwa na umwagikaji wa damu. Sikutaka kuingia Ikulu kupitia damu za watu kwa sababu sistahili hivyo,” alisema. Hata hivyo, alisema licha ya uchaguzi huo kutoaminika, bado anamheshimu Dk Magufuli kama Rais, japo mbunge huyo wa zamani wa Monduli alikataa kukubaliana na utendaji wa mkuu huyo wa nchi kwa kipindi alichokaa madarakani. “Hata kama Dk Magufuli alichaguliwa katika mfumo usioaminika wa uchaguzi, bado tunamheshimu kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Lowassa. Alisema, “Utendaji wa Rais Magufuli utaamuliwa na watu utakapofika mwisho wa muhula huu mwaka 2020. Bora niwe makini katika hili nisije nikanukuliwa vibaya nikaingia kwenye matatizo nitakaporudi nyumbani.” Lowassa ambaye hivi karibuni amekuwa akiripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kutokana na kauli yake kuhusu viongozi wa Jumuiya ya Uamsho waliokamatwa mwaka 2012 huko Zanzibar,JE UTAMPA KURA YAKO??...COMMENT YES OR NO??