Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JUST IN: Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na kampuni ya Tigo kupinga kuwalipa wasanii AY na MwanaFA Tshs 2,185,000,000 kwa kutumia nyimbo zao bila kulipa. Wakili Albert Msando ambaye anawakilisha wasanii hao amesema huu ni ushindi muhimu kwa sanaa ya Tanzania. Amenukuliwa akisema "ni haki yao kulipwa kwa sababu ni kazi zao ambazo zinalindwa kisheria".
 
Jana jioni Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge kutokea mkoa wa Singida Tundu Lissu alikamatwa na Polisi uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa anaelekea Rwanda ambapo alichukuliwa na kuendelea kushikiliwa na Polisi hadi leo. Taarifa ambayo imetolewa mchana huu na Afisa habari wa CHADEMA ni kwamba Polisi wamemchukua Tundu Lissu kutoka kituo kikuu cha polisi na wanaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kupekuliwa ambapo taarifa hiyo ya CHADEMA imesema hadi muda inapotolewa taarifa hii haujajulikana upekuzi huo unahusu kitu gani. .
 
Licha ya ukaribu wao kuchukuliwa kama kiki, msanii Harmorapa amezidi kusisitiza yupo katika mahusiano ya kimapenzi na video vixen Amber Lulu licha ya mrembo huyo kuwahi kukanusha hilo. Harmorapa ambaye amekuwa akivutia watu wengi kwa vituko vyake, ameiambia Boys Boys ya TV1 kuwa yeye kama kijana wa kiume ni lazima awepo katika mahusiano. “Unajua siku zote kama ni mwanaume, halafu mwanaume rijali ni lazima uwe kwenye mahusiano ya kimapenzi, kwa hiyo mimi nina mpenzi, kuoa bado hata mtoto sina. Kwa sasa ni mtu famous, nilishamtaja ili kuna wengine hawamfahamu ni Amber Lulu,” amesema Harmorapa. . .
 
KIMENUKAAA... @barakahtheprince_ amefunguka kuwa amejitoa rasmi kwenye Lebo ya Rockstar 4000 ambayo ilikuwa ikisimamia kazi zake za Muziki kwa miezi kadhaa nyuma! Baraka amedai hakuna maelewano mazuri baina yake na Uongoza wa Rockstar 4000 ndio sababu amefikia maamuzi ya kujitoa kwenye Lebo hiyo! . .
 
Muzee ya kutafuta kiki kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…