Uzi maalum wa nyau wetu majumbani

Wala siwaelewi, japo nafuga paka na ninaye mkongwe na anajua akiskia sauti ya mfuko anajua ni menyu time, ila sio km ananipenda lah hasha anapenda chake kiwepo, na bado nasimamia palepale paka hafundishiki, nimekaa naye miaka 9 haelewi kitu. He is just broken
 

Unaweza ukawa umekaa nae hata miaka 15 ila kama haujaonyesha nia ya kumfundisha aelewe nini sahihi cha kufanya basi sahau mkuu utamuona kama mzigo tu. Labda haujajua tu njia gani za kumfundisha akuelewe na atii kila unapotaka afanye ulilomfundisha. Paka hafundishi kwa maneno anafundishwa kwa vitendo na lazima awe sehemu ya tukio unalotaka afanye anachopaswa kufanya ndo atakuelewa japo itachukua hata wiki mbili kuanza kuelewa vyema na kuhifadhi kwenye kumbukumbu zake. kuhusu kula sio paka tu hata mbwa nao wameumbwa na asili ya kula kula tu sasa kama amehisi kuna kitu cha kula kinanukia kwa nini asiombe apewe? kumbuka wana uwezo mkubwa pia wa kunusa.
 
Na sisi masela tunaokaa ghetto tunacomment wapi?
Maana paka hawezi kukaa ghetto atakufa njaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…